-
Mapinduzi ndani ya utawala wa kifalme Saudia yaendelea, mtoto mdogo wa Mfalme Salman ateuliwa kuwa balozi wa Riyadh huko Marekani
Jul 23, 2017 03:03Ndugu yake mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia na mtoto mdogo wa Mfalme wa sasa wa nchi hiyo usiku wa kuamkia leo amekabidhi hati zake za utambulisho kwa Rais Donald Trump wa Marekani kama balozi mpya wa Saudia nchini humo.
-
Kuanzishwa taasisi mpya ya usalama na kuzidi kujiimarisha Mohammed bin Salman nchini Saudia
Jul 22, 2017 01:24Mfalme Salman bin Abdulaziz Aal Saud wa Saudi Arabia Alkhamisi usiku alitoa amri ya kuundwa taasisi mpya ya usalama nchini humo suala ambalo linahesabiwa na wachambuzi wa mambo kwamba limefanyika kwa nia ya kumtia nguvu mwanawe yaani Mohammed bin Salman, mrithi mpya wa kiti cha ufalme wa nchi hiyo.
-
Ugonjwa wa kipindupindu Yemen ni mbaya zaidi katika historia ya dunia
Jul 21, 2017 21:59Shirika la kutoa misaada la Oxfam linasema mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu Yemen ni mbaya zaidi katika historia ya zama hizi duniani. Kipindupidu kimeenea Yemen kufuatia hujuma ya kijeshi na mzingiro wa Saudia dhidi ya nchi hiyo.
-
Kuua wapinzani, silaha ya kisiasa inayotumiwa kwa ajili ya malengo ya kimadhehebu Saudi Arabia
Jul 20, 2017 03:09Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limekutaja kuua raia kuwa ni silaha ya kisiasa inayotumiwa na utawala wa Saudi Arabia kwa ajili ya kuwanyamazisha wapinzani wake.
-
Mwandishi wa Algeria: Saudia ni silaha inayotumiwa na Marekani kuwahujumu Waislamu
Jul 19, 2017 12:49Mwandishi maarufu wa nchini Algeria Haddat Hizam, amesema kuwa kinyume na madai yanayotolewa, Saudia si tu kwamba haina na nafasi yoyote yenye maslahi katika eneo, bali ni nyenzo bora inayotumiwa na Marekani kuwalenga Waislamu.
-
Wasudan elfu 50 watimuliwa Saudia kwa sababu ya matatizo ya kiuchumi ya Riyadh
Jul 18, 2017 11:04Jumla ya Wasudan elfu 50 wanaoishi nchini Saudia, wametakiwa kuondoka nchi hiyo kabla ya muda waliopewa na serikali ya Riyadh kumalizika.
-
Saudia yaichochea FIFA iipokonye Qatar uwenyeji wa Kombe la Dunia 2022
Jul 16, 2017 02:31Saudi Arabia inaziongoza nchi kadhaa za Kiarabu katika kulishinikiza Shirikisho la Soka Duniani kuipokonya Qatar haki ya kuandaa Kombe la Dunia mwaka 2022 kwa madai kuwa nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi inaunga mkono ugaidi.
-
Saudia yashindwa kuishawishi OIC kutoa azimio dhidi ya Iran
Jul 14, 2017 22:03Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Kisiasa na Usalama wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, pendekezo la Saudia la kuingizwa kipengee cha kuilaani Iran katika taarifa ya mwisho ya kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC limetupiliwa mbali na wajumbe wa kikao hicho.
-
Maafisa wa Saudia waliwasaidia magaidi wa ISIS huko Mosul, Iraq
Jul 14, 2017 03:33Saudi Arabia ilituma maafisa wake wa kijasusi na kijeshi kujiunga na magaidi wa ISIS au Daesh Mosul wakati wa oparesheni ya jeshi la Iraq ya kuukomboa mji huo.
-
Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Uingereza wazidi kulalamikiwa kimataifa
Jul 12, 2017 03:02Taasisi za kutetea haki za binadamu nchini Uingereza zimekosoa kuendelea mchakato wa kuiuzia silaha Saudi Arabia ili izitumie katika mashambulizi yake dhidi ya raia wa Yemen wasio na hatia.