-
UN yaiondoea vikwazo vya silaha Somalia, yahitimisha shughuli zake za kisiasa nchini Sudan
Dec 02, 2023 05:59Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio la kuondoa vikwazo vya mwisho vya silaha dhidi ya serikali ya Somalia na vikosi vyake vya usalama, huku likihitimisha pia shughuli za ujumbe wake wa kisiasa katika nchi ya Sudan iliyokumbwa na vita.
-
UN yatoa indhari: Idadi ya wanaokimbilia Sudan Kusini kutoka Sudan imeongezeka
Nov 10, 2023 06:56Mashirika ya kibindamu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini yametahadharisha kuhusu ongezeko kubwa la watu wanaorejea na wakimbizi wanaokimbia mzozo na kuelekea kaskazini nchini Sudan.
-
Familia za Wasudan zatafuta hifadhi Sudan Kusini
Oct 27, 2023 13:09Ripoti zinasema kuwa katika hali ya kusikitisha, familia zinazoepuka ghasia na machafuko nchini Sudan zinaendelea kuwasili katika maeneo ya mbali ya kaskazini mwa Sudan Kusini.
-
UNHCR: Watu elfu nne wameuliwa Darfur, Sudan, mali za raia zimeharibiwa
Oct 18, 2023 03:50Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema, watu wapatao 4,000 wameuawa huku mali za raia zikiharibiwa katika mapigano yanayoendelea huko jimboni Darfur nchini Sudan, mapigano ambayo yalianzia kwenye mji mkuu Khartoum miezi sita iliyopita na kusambaa hadi nje ya mji huo, kati ya Jeshi la Serikali (SAF) na wanamgambo wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF).
-
Salva Kiir kuwa mwenyeji wa viongozi wa Sudan kujadili amani
Oct 17, 2023 14:12Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amesema karibuni hivi atakuwa mwenyeji wa mkutano utakaowaleta pamoja viongozi wa pande mbili zinazopigana nchini Sudan, yaani Jeshi la Taifa la Sudan (SAF) na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF)
-
Iran na Sudan kufungua tena balozi zao baada ya kukamilisha mchakato wa kuhuisha uhusiano
Oct 10, 2023 07:04Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, karibuni hivi Iran na Sudan zitafungua tena balozi zao baada ya nchi hizo mbili kukamilisha mchakato wa kurejesha uhusiano wa kidipolmasia.
-
UN: Mapigano Sudan yanasababisha kuongezeka kwa kasi mgogoro wa wakimbizi duniani
Oct 06, 2023 03:27Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu huko Sudan amesema kuwa mapigano yanayoendelea nchini humo yanapelekea kuongezeka haraka mgogoro unapanuka wa wakimbizi duniani.
-
Sudan Kusini: Benki ya BRICS ni mwanzo wa mwisho wa udhibiti wa sarafu ya dola
Sep 30, 2023 15:44Waziri wa Mambo ya Rais wa Sudan Kusini amesema kuwa, kudhihiri kwa Benki mpya ya NDB ya kundi la madola yanayoinukia kiuchumu la BRICS utakuwa mwanzo wa kusambaratika udhibiti wa sarafu ya dola ya Marekani katika miamala ya kifedha duniani kote.
-
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC: Najisikia aibu hatujafanya kazi nzuri huko Sudan
Sep 28, 2023 02:59Karim Khan, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) amezungumza na televisheni ya France 24 pambizoni mwa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York akikiri kwamba taasisi hiyo haijafanya kazi nzuri kuhusiana na yanayojiri nchini Sudan.
-
OCHA: Mamilioni ya Wasudan wamekuwa wakimbizi kutokana na kuendelea vita na mapigano
Sep 24, 2023 03:15Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa mamilioni ya watu wamelazimika kuyahama makazi yao na kuwa wakimbizi kutokana na kuendelea vita na mapigano kati ya Jeshi na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka, RSF nchini Sudan.