-
Rais Assad arejesha nishani aliyopewa na 'Mtumwa wa Marekani'
Apr 20, 2018 02:54Rais Bashar al Assad wa Syria amerejesha nishani bora zaidi ya Ufaransa aliyotunukiwa na Rais Jacques Chirac mwaka 2001 na kusema hawezi kubakia na zawadi ya nchi ambayo ni mtumwa wa Marekani na ambayo imedondosha mabomu Syria.
-
Velayati: Baada ya muda si mrefu Yemen pia itajumuishwa kwenye kambi ya Muqawama
Apr 19, 2018 23:49Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema: kambi ya muqawama imepanuka kwa kuanzia Iran na kuenea hadi Palestina, Syria na Iraq; na muda si mrefu Yemen pia itajumuishwa kwenye kambi hiyo.
-
Russia: Makundi ya kigaidi Syria yanawazuia wakaguzi wa OPCW kuingia Douma
Apr 19, 2018 09:57Nabu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na nchi za kigeni huko Syria yanawazuia wakaguzi wa Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali (OPCW) kuingia katika mji wa Douma ulioko katika viunga ya mji mkuu wa nchi hiyo, Damascus.
-
CNN yafichua: Shambulio dhidi ya Syria lilifanywa bila kuwepo uhakika kama silaha za kemikali zilitumiwa Duma
Apr 18, 2018 22:33Ukiwa umepita muda wa chini ya wiki moja tangu Marekani na waitifaki wake waishambulie kijeshi Syria kwa madai ya kufanyika shambulio la silaha za kemikali nchini humo, kanali ya televisheni ya CNN ya nchini Marekani imefichua kuwa nyaraka na ushahidi uliotumiwa kwa ajili ya shambulio hilo ni picha tu na sampuli za vipimo visivyo vya moja kwa moja.
-
Magaidi elfu tano (5000) walazimika kuondoka katika viunga vya mji mkuu wa Syria
Apr 18, 2018 22:33Hatimaye, genge la kigaidi la Jeish al Islam limetangaza kuwa limekubali kuondoa wanamgambo wake 5,000 waliko katika eneo la al Dhamir katika viunga vya mji mkuu wa Syria Damascus na kuwapelekea Jarabulus mkoani Halab (Aleppo) pamoja na familia zao.
-
Rouhani: Iran na Uturuki zitaendelea kushirikiana ili kuzima taharuki Syria
Apr 18, 2018 03:00Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema mashambulizi ya hivi karibuni ya kijeshi yaliyofanywa na Marekani, Uingereza na Ufaransa dhidi ya Syria yameacha mfano wenye sura ya kutisha kwenye uhusiano wa kimataifa, na kusisitiza kwamba Iran na Uturuki zitaendelea kuwa na ushirikiano wa karibu kwa lengo la kuzuia kushtadi taharuki katika nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Wayemen waandamana kuiunga mkono serikali ya Syria
Apr 17, 2018 23:44Mamia ya Wayemen wamefanya maandamano na kukusanyika mbele ya ubalozi wa Syria na Chuo Kikuu cha Sana'a, wakionyesha mshikamano wao na serikali halali ya Syria, chini ya uongozi wa Rais Bashar al-Assad wa nchi hiyo.
-
Jeremy Corbyn: Ishambulieni Saudia pia kwa kuwa imetumia silaha za sumu Yemen
Apr 17, 2018 23:32Kiongozi wa chama cha Leba nchini Uingereza ametaka kufanywa mashambulizi ya anga kuilenga Saudia kutokana na nchi hiyo ya Kiarabu kutumia mabomu yaliyopigwa marufuku na Umoja wa Mataifa dhidi ya raia wasio na hatia nchini Yemen.
-
Russia: Madai ya shambulizi la silaha za kemikali Syria yaliratibiwa na majasusi wa Uingereza
Apr 17, 2018 09:54Mwakilishi wa Russia katika Shirika Linalopiga Marufuku Matumizi ya Silaha za Kemikali (OPCW) amesema madai ya kutumiwa silaha za kemikali katika eneo la Douma nchini Syria na yaliyotumika kama kisingizio cha kuishambulia nchi hiyo ya Kiarabu, ni operesheni ya mchezo mchafu iliyopangwa na kutekelezwa na asasi za kijasusi za Uingereza.
-
Syria: Hivi sasa tuna uwezo mkubwa wa kutungua makombora ya adui
Apr 17, 2018 09:51Mshauri wa Rais Bashar al-Assad wa Syria, Bouthaina Shaaban amesema kuwa, jeshi la Syria limethibitisha uwezo mkubwa wa makombora yake hasa baada ya kukabiliana vilivyo na shambulizi la hivi karibuni la Marekani, Uingereza na Ufaransa dhidi ya nchi hiyo.