Wayemen waandamana kuiunga mkono serikali ya Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i43276-wayemen_waandamana_kuiunga_mkono_serikali_ya_syria
Mamia ya Wayemen wamefanya maandamano na kukusanyika mbele ya ubalozi wa Syria na Chuo Kikuu cha Sana'a, wakionyesha mshikamano wao na serikali halali ya Syria, chini ya uongozi wa Rais Bashar al-Assad wa nchi hiyo.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Apr 17, 2018 23:44 UTC
  • Wayemen waandamana  kuiunga mkono serikali ya Syria

Mamia ya Wayemen wamefanya maandamano na kukusanyika mbele ya ubalozi wa Syria na Chuo Kikuu cha Sana'a, wakionyesha mshikamano wao na serikali halali ya Syria, chini ya uongozi wa Rais Bashar al-Assad wa nchi hiyo.

Maandamano hayo yaliyowashirikisha wanasiasa, shakhsia mbalimbali, wamiliki wa vyombo vya habari na wanafikra wa nchi hiyo, yameitishwa kwa ajili ya kulaani hujuma za makombora za Marekani, Uingereza na Ufaransa za hivi karibuni dhidi ya taifa hilo la Kiarabu. Khalid al-Sabai, kiongozi wa kundi la kisiasa la 'Muungano wa Pamoja' amewambia waandishi wa habari na washiriki wa maandamano hayo kwamba, hii leo muhimili imara wa muqawama unaendelea kuanzia Tehran, Sana'a, Bairut na Baghdad na kwamba kamwe hautorudi nyuma. Naye kwa upande wake, Abdul-Fattah Haifarah, mmoja wa wanaharakati wa vyombo vya habari nchini Yemen amesema kuwa, Wayemen wanawaunga mkono Wasyria katika muqawama na mapambano yao dhidi ya mashambulizi ya Marekani, Israel na washirika wao dhidi ya nchi yao.

Maandamano ya kuiunga mkono serikali ya Syria yameshuhudiwa hadi nchini Marekani

Kadhalika washiriki wa maandamano hayo wamesisitiza juu ya udharura wa kukabiliana na tawala wa kidikteta za Kiarabu ambazo kwa sasa zimekuwa mstari wa mbele katika kuboresha uhusiano wao na utawala haramu wa Israel. Jumamosi asubuhi, Marekani, Uingereza na Ufaransa ziliishambulia kwa makombora Syria, mashambulizi ambayo hata hivyo hayakuwa na taathira yoyote. Maandamano ya kupinga hujuma za muungano wa Kimagharibi dhidi ya Syria, yameshuhudiwa katika nchi mbalimbali za dunia zikiwemo za Marekani, Ulaya na Kiarabu.