-
Malori ya misaada yasubiri 'idhini ya Israel' Rafah ili yaingie Gaza
Oct 16, 2025 01:54Gavana wa Sinai Kaskazini nchini Misri amesema mamia ya malori ya misaada yapo tayari kuingia katika Ukanda wa Gaza kupitia kivuko cha Rafah, lakini yanasubiri kibali cha utawala wa Israel ili yaingize misaada hiyo ya dharura.
-
Israel yaua Wapalestina wengine 6 huko Gaza; Hamas yalalamikia kukiukwa usitishaji vita
Oct 14, 2025 09:23Jeshi la Israel limewauwa shahidi takriban Wapalestina sita huko Ukanda wa Gaza ndani ya saa 24, licha ya Tel Aviv hivi karibuni kufikia makubalianokuhusu utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mpango wa kusitisha vita.
-
HAMAS: Tony Blair hakaribishwi kuwa na nafasi yoyote katika uongozi wa Ghaza baada ya vita
Oct 12, 2025 02:14Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imeonya kwamba Tony Blair hatakaribishwa kuwa na nafasi yoyote ya uendeshaji wa Ghaza kufuatia kuanza kutekelezwa usitishaji vita katika eneo hilo la Palestina.
-
"Israel haiaminiki; Iran inaunga mkono kusimamishwa mauaji ya kimbari Gaza"
Oct 11, 2025 23:29Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi amesema Jamhuri ya Kiislamu inakaribisha kusitishwa kwa mauaji ya kimbari ya utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza, huku akitoa indhari juu ya tabia ya kutokuwa na muamana Tel Aviv kwa kukiuka makubaliano kadhaa ya huko nyuma.
-
Iran: Tunaunga mkono mpango wowote wa kumaliza vita, mauaji ya kimbari Gaza
Oct 09, 2025 23:51Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesisitiza kwa mara nyingine tena kwamba Jamhuri ya Kiislamu daima inaunga mkono mpango wowote unaolenga kukomesha vita na mauaji ya halaiki huko Gaza, na kusisitiza ulazima wa kuwa macho mkabala wa hulka ya utawala wa Israel ya kukiuka ahadi na makubaliano.
-
WHO: Watu 400 wameaga dunia kwa utapiamlo Ukanda wa Gaza tangu kuanza mwaka huu
Oct 06, 2025 08:13Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti kuwa watu 400 wameaga dunia kw autapiamlo katika Ukanda wa Gaza kutokana na njaa ya makusudi iliyosaabishwa na Israel. Watoto 100 ni miongoni mwa idadi hii tajwa ya waliopoteza maisha kwa njaa; watoto 80 walikuwa na umri wa chini ya miaka mitano.
-
Wakfu wa Mandela walaani shambulio la Israel dhidi ya msafara wa Sumud
Oct 05, 2025 07:11Wakfu wa Nelson Mandela, taasisi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa kwa ajili ya kumbukumbu ya rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, imelaani amelaani vikali shambulio la utawala wa Israel dhidi ya msafara wa kimataifa wa meli nyingi wa Sumud uliokuwa ukielekea Ukanda wa Gaza, na kutaka kuachiwa mara moja kwa wanaharakati waliotekwa nyara na kuzuiliwa na askari wa majini wa Kizayuni.
-
Israel yampuuza Trump, yaendelea kuwaua Wapalestina Gaza; Hamas yalaani
Oct 04, 2025 23:17Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imemjia juu Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa madai ya uwongo kuwa ameliamuru jeshi la utawala huo kupunguza mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza.
-
Pakistan: Mpango wa Trump kuhusu Ghaza ni tofauti na ulioidhinishwa na viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu
Oct 03, 2025 07:04Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Ishaq Dar amesema mpango wa amani wa vipengele 20 uliopendekezwa na Rais wa Marekani Donald Trump kwa ajili ya Ghaza sio ule ulioidhinishwa na viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu, ikiwemo Pakistan.
-
Jihadul Islami, Ansarullah zapinga mpango wa Trump-Netanyahu kuhusu Gaza
Oct 01, 2025 07:21Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Jihadul Islami ya Palestina amekosoa vikali mpango wa Rais Donald Trump wa Marekani wenye vipengele 20 wa eti kumaliza vita vya mauaji ya halaiki ya Israel dhidi ya Gaza, na kuutaja kama "mfumo wa kuendeleza uchokozi na uvamizi wa Israel dhidi ya taifa la Palestina."