Pars Today
Huku akielezea malengo ya safari yake ya siku tatu nchini Iraq, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian amesema kuwa: Lengo kuu la serikali ni umoja, mafungamano na maelewano katika Umma mzima wa Kiislamu.
Rais wa Iran, Ebrahim Raisi, amesema ni wajibu wa kibinadamu na kidini kwa nchi za Kiislamu kukomesha mauaji ya kimbari ya miezi kadhaa ya utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina huko Gaza.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Ahul Bayt AS- yaani watu wa nyumba ya Mtume Muhammad SAW, ni ufunguo wa Umoja wa Kiislamu na chimbuko la matumaini katika jamii ya mwanadamu.
Katibu Mkuu wa harakati ya Ansurulla nchini Yemen amesema kuwa Uislamu wa Kimarekani, Kisaudia na Kiimarati ni Uislamu wa kinafiki unaopingana na asili ya Uislamu.
Alimu mmoja wa ngazi ya juu wa Kiislamu nchini Tunisia, amesema kuwa fatwa za upotoshaji za mamufti wa Saudia, zinaelekea kuuangamiza umma wa Kiislamu.
Mkuu wa Taasisi ya Wakfu na Mambo ya Kheri ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, siasa kuu za Tehran ni kupigania umoja na mshikamano katika umma wa Kiislamu.
Kongamano la sita la "Umoja wa Umma wa kiislamu Katika Kukabiliana na Utakfiri" lilifanyika jana Jumamosi katika mji wa Bojnord kaskazini mashariki mwa Iran na kuhudhuriwa na mamia ya wasomi wa madhehebu ya Kishia na Kisuni.
Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen imesisitiza juu ya udharura wa kutumiwa mafundisho ya Bwana Mtume (saw) kwa ajili ya kukabiliana na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel tawala mbazo ni maadui wa Umma wa Kiislamu.
Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ni Siku ya Kimataifa ya Quds. Hiyo ni siku ya mwamko wa Umma wa Kiislamu mbele ya dhulma, ukandamizaji na utumiaji mabavu wa mababeru.