-
New York Times: Jeshi la Israel liliidhinisha kuuliwa raia mpaka 100 Ghaza ili kumpata mshukiwa mmoja wa Hamas
Dec 27, 2024 04:13Uchunguzi uliofanywa na gazeti la New York Times la Marekani unaonyesha kuwa, jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel lililegeza kwa kiwango kikubwa sheria zake za kivita katika miezi ya mwanzo ya vita vyake dhidi ya Ghaza, na kusababisha vifo vingi vya raia.
-
Iraq yafukua mabaki ya miili 100 ya Wakurdi wanawake na watoto waliouliwa na Saddam
Dec 27, 2024 03:55Mamlaka ya Iraq imeanza kufukua mabaki ya miili ya wanawake na watoto wapatao 100 wa Kikurdi walioripotiwa kuuliwa na utawala wa Saddam Hussein katika miaka ya 1980.
-
Polisi ya Kenya 'yasutwa' kwa kudai hakuna Wakenya waliotekwa nyara
Dec 27, 2024 03:54Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu ya Kenya (KNCHR) imekanusha ripoti ya Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja kwamba hakuna Wakenya waliotekwa nyara nchini humo ikisema, katika mwezi huu wa Desemba pekee, watu saba hasa watumiaji wa mitandao ya kijamii wametekwa nyara; na kufikia sasa, sita hawajulikani waliko.
-
Licha ya hujuma za kinyama za Israel Sana'a na Hudaydah, kombora jengine la Yemen lapiga Tel Aviv
Dec 27, 2024 00:08Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimeripoti kuwa ving'ora vya tahadhari ya mashambulio ya anga vimesikika katika sehemu kubwa ya maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu yaliyopachikwa jina bandia la Israel kufuatia shambulio la kombora lililorushwa kutoka Yemen mapema leo.
-
Hamaki ya Tel Aviv dhidi ya matamshi ya Papa kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni
Dec 26, 2024 10:08Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya utawala wa Kizayuni wa Israel imemwita balozi wa Vatican katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu kwa ajili ya kusailiwa. Ni baada ya Papa Francis, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani kukosoa vita na mauaji ya Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
Barua ya Iran kwa Baraza la Usalama baada ya Israel kukiri ilihusika na mauaji ya Ismail Haniyeh
Dec 25, 2024 08:37Amir Saeid Iravani, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa jana Jumanne alimwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akisisitiza kwamba, Israel imebeba dhima ya kuhusika na mauaji ya Shahidi Ismail Haniyeh, mkuu zamani wa Idara ya Siasa ya harakati ya Hamas.
-
Maulamaa wa Yemen wautaka Umma wa Kiislamu kukabiliana na mashambulizi ya Wazayuni na Marekani
Dec 25, 2024 00:18Maulamaa wa Yemen wameutaka Umma wa Kiislamu kukabiliana na mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Isreal na Marekani huko Gaza, Yemen na pia waungaji mkono wa kigaidi.
-
HAMAS: Wapalestina wapambane kuondoa mzingiro wa kinyama uliowekwa na Mamlaka ya Palestina
Dec 24, 2024 08:19Afisa mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ametoa wito wa kufanyika "hamasa kubwa ya umma" kwa lengo la kuondoa mzingiro wa kinyama uliowekwa na Mamlaka ya Ndani ya Palestina (PA) kwenye kambi ya wakimbizi ya Jenin, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
-
Wazayuni wayafanya maisha kuwa magumu huko Jabalia, Ukanda wa Gaza
Dec 23, 2024 10:31Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wameifanya hali ya mambo na maisha kuwa ngumu katika eneo la Jabalia kwa lengo la kuwahamisha kwa nguvu wakazi wa Kipalestina wa mji huo.
-
Mjumbe wa Ansarullah: Utawala wa Kizayuni hauna ubavu wa kukabiliana na vikosi vyetu peke yake
Dec 23, 2024 02:20Mjumbe Mwandamizi wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza kwa kusema: "mashambulizi yetu yaliukanganya mfumo wa ulinzi wa anga wa Marekani na kupelekea kutunguliwa ndege ya kivita ya Marekani kwa shambulio lao wenyewe" na akaongeza kuwa utawala wa Kizayuni hauna ubavu wa kukabiliana na Wayemen peke yake na ndio maana unaomba msaada kwa watu wanaouunga mkono.