OIC leo inajadili mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza na kuunganisha pamoja misimamo
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i129958-oic_leo_inajadili_mauaji_ya_kimbari_ya_israel_huko_gaza_na_kuunganisha_pamoja_misimamo
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) wanafanya mkutano wa dharura leo Jumatatu katika mji wa Jeddah nchini Saudi Arabia kujadili vita vya mauaji ya kimbari vya Israel huko Gaza na kuunganisha misimamo yao kuhusu mauaji yanayofanywa na Israel katika ukanda huo.
(last modified 2025-08-25T02:59:12+00:00 )
Aug 25, 2025 02:59 UTC
  • OIC leo inajadili mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza na kuunganisha pamoja misimamo

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) wanafanya mkutano wa dharura leo Jumatatu katika mji wa Jeddah nchini Saudi Arabia kujadili vita vya mauaji ya kimbari vya Israel huko Gaza na kuunganisha misimamo yao kuhusu mauaji yanayofanywa na Israel katika ukanda huo.

Taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki ilieleza kuwa mkutano huo utajadili mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi ya watu wa Palestina na uamuzi wa Israel wa kupanua operesheni zake huko Gaza.

Mkutano wa Jeddah unatarajiwa kuongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, rais wa sasa cha Baraza hilo.

Awali, katika taarifa yake ya pamoja na Kundi la Waarabu katika Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), ilikuwa imelaani tangazo la Israel la nia yake ya kulikalia kwa mabavu eneo lote la Ukanda wa Gaza, na kuitaja hatua hiyo kuwa ni "ongezeko hatari na lisilokubalika," na kutoa wito wa kuruhusiwa misaada kuingia eneo hilo mara moja.

Kabla ya kuelekea Jeddah kwa ajili ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa OIC, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamuu, Abbas Araqchi alitahadharisha kuwa njozi za kile kinachoitwa "Israel Kubwa" inawakilisha hatari na tishio kubwa kwa amani na usalama wa dunia. Araqchi amezitolea wito nchi za Kiislamu kuchukua hatua za pamoja za kukabiliana na ajenda ya kujitanua ya Israel.

"Mkutano ujao wa Mawaziri wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) haupasi kuishia tu katika kutoa matamko ya mshikamano na watu wa Palestina au kueleza kusikitishwa nahali ya sasa", alisema Araqchi katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Sayyid Abbas Araqchi aliutaja mkutano huo wa OIC kuwa ni "mtihani wa kihistoria kwa Umma wa Kiislamu na labda mojawapo ya fursa chache za kuunda muungano wa kikanda na kimataifa ili kukomesha uvamizi wa Israel."