Ansarullah: Wazayuni wawafanyia ukatili hata wanawake wajawazito
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i134164-ansarullah_wazayuni_wawafanyia_ukatili_hata_wanawake_wajawazito
Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen, ametoa hotuba kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake na kugusia jinsi utawala wa Kizayuni wa Israel unavyoua kikatili maelfu ya wanawake Waislamu nchini Palestina wakiwemo wanawake wajawazito, wazee na watoto na kusema kuwa, Wazayuni hawawaonei huruma hata wanawake wajawazito na vitoto vichanga vilivyomo tumboni.
(last modified 2025-12-11T03:36:14+00:00 )
Dec 11, 2025 03:36 UTC
  • Ansarullah: Wazayuni wawafanyia ukatili hata wanawake wajawazito

Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen, ametoa hotuba kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake na kugusia jinsi utawala wa Kizayuni wa Israel unavyoua kikatili maelfu ya wanawake Waislamu nchini Palestina wakiwemo wanawake wajawazito, wazee na watoto na kusema kuwa, Wazayuni hawawaonei huruma hata wanawake wajawazito na vitoto vichanga vilivyomo tumboni.

Sayyid "Abdul Malik Badreddin Al-Houthi" alisema hayo jana Jumatano jioni kwa mnasaba wa "Siku ya Kimataifa ya Wanawake Waislamu" akisisitiza kwamba, matokeo ya jinai hizo za Wazayuni ni kuzidi kufedheheka Israel na waungaji mkono wake na wajibu kwa Waislamu kuachana na fikra potofu za kuwa tegemezi kwa madola ya kibeberu.

Mwanzoni mwa hotuba yake, Al Houthi amesema kuwa, umma wa Kiislamu umekumbwa na vita laini ambavyo ni hatari zaidi kuliko vita vya silaha na madhara yake ni mazito zaidi. Hali hiyo imepelekea baadhi ya Waislamu kutangatanga na kuwatii maadui na kuna ushahidi wa wazi wa uhakika huo.

Kiongozi huyo wa harakati ya Ansarullah ya Yemen ameelezea kusikitishwa sana na namna madola ya kibeberu yalivyopewa nafasi ya kuwa na "ushawishi mkubwa katika Ulimwengu wa Kiislamu," akisema kwamba, maadui "wamechukua udhibiti wa tawala nyingi za nchi za Waislamu."

Amesema: "Utajiri wa nchi za Kiislamu umekuwa chanzo cha mapato ya madola ajinabi, ardhi za Waislamu zimekuwa vituo vya kijeshi vya madola ya kigeni na rasilimali watu za nchi za Waislamu zinatumika kuwahudumia na kuwatii maadui." 

Sayyid Abdul Malik Al-Houthi aidha amesema: “Leo hii adui Mzayuni amekuwa na kiburi kikubwa kiasi kwamba anajaribu kulazimisha Waislamu wakubali damu zao, ardhi zao, maeneo yao matakatifu na hata dini yao kuwekwa rehani ya kukwepa kushambuliwa na Israel." Amesema: “Wamarekani pia ni washirika katika jinai hizo na wanajaribu kuwalazimisha Waislamu kuwa dhalili kiasi hicho.”