Haniya: Haiwezekani kutenganisha baina ya Gaza na Ukingo wa Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i31676-haniya_haiwezekani_kutenganisha_baina_ya_gaza_na_ukingo_wa_magharibi
Mkuu wa Idara ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa, harakati hiyo iko tayari kukomesha mgawanyiko ulioko huko Palestina na kwamba eneo la Gaza kamwe halitatenganishwa na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 12, 2017 10:01 UTC
  • Haniya: Haiwezekani kutenganisha baina ya Gaza na Ukingo wa Magharibi

Mkuu wa Idara ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa, harakati hiyo iko tayari kukomesha mgawanyiko ulioko huko Palestina na kwamba eneo la Gaza kamwe halitatenganishwa na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Ismail Haniya amesema kuwa, Hamas inafanya jitihada za kuhakikisha kunapatikana mapatano ya kitaifa, serikali ya umoja wa kitaifa na kuitishwa uchaguzi wa bunge, na inataka kuunganishwa tena maeneo ya Gaza na Ukingo wa Magharibi. 

Mkuu wa Idara ya Siasa ya Hamas ameongeza kuwa, haiwezekani kutetea Palestina bila ya kuwepo ushirikiano na juhudi za pande na makundi yote.

Ismail Haniya

Ismail Haniya amesema kuwa, Palestina ni kadhia ya Umma wa Kiislamu na Kiarabu na kwamba, inapaswa kuwekwa mbali na mivutano ya sasa katika eneo la Mashariki ya Kati.