-
Zaidi ya 70% ya Wapalestina wanapinga HAMAS kukabidhi silaha kabla Israel kuondoka kikamilifu Ghaza
Aug 15, 2026 03:49Uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa na Kituo cha Utafiti wa Sera na Utafiti cha Palestina (Palestinian Center for Policy and Survey Research) unaonyesha kuwa, zaidi ya asilimia 70 ya Wapalestina wanapinga Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina, HAMAS kukabidhi silaha zake kabla utawala wa kizayuni wa Israel kuondoka kikamilifu katika Ukanda wa Ghaza.
-
Muqawama wa Palestina watoa onyo baada ya mashambulizi mabaya zaidi ya Israel tangu kusitisha mapigano
Aug 03, 2026 10:10Makundi ya Muqawama ya Palestina yametoa onyo kali baada ya mashambulizi mabaya zaidi ya anga ya Israel tangu kusitisha mapigano Oktoba 2025, yakisema mashambulizi hayo yasiyokoma ni hujuma ya makusudi dhidi ya makubaliano ya kusitisha mapigano na ujumbe kwamba Israel haina nia ya kutimiza majukumu yake.
-
Shambulio la Israel dhidi ya maghala ya dawa Ghaza latajwa kuwa ni 'jinai ovu sana'
Aug 02, 2026 02:42Wizara ya Afya ya Ghaza imelaani kile ilichokiita "jinai ovu sana" iliyofanywa na vikosi vya utawala wa kizayuni wa Israel huko Deir el-Balah, ikisema shambulio hilo la Ijumaa asubuhi lililenga "maghala ya dawa" ya Hospitali ya Mashahidi wa Al-Aqsa, na kuyabomoa kikamilifu mawili kati ya maghala hayo.
-
Hamas: Kuongezeka mashambulizi dhidi ya Gaza ni jaribio la kuua makubaliano ya kusitisha mapigano
Jul 24, 2026 07:13Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetangaza kwamba mashambulizi makubwa ya anga ya utawala wa Israel eneo la Ukanda wa Gaza katika saa kadhaa zilizopita ni mwendelezo wa vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya raia wasio na hatia na msisitizo wa kuvuruga makubaliano ya kusitisha mapigano.
-
Israel yafanya mauaji makubwa huko Nuseirat, janga la binadamu linazidi kuwa baya Gaza
Jul 18, 2026 10:59Wapalestina 14 wameuawa na wengine 37 kujeruhiwa, wengi wao wakiwa katika kambi ya Nuseirat katikati mwa Ukanda wa Gaza, kutokana na mashambulizi mtawalia ya Israel yaliyolenga maeneo mbalimbali ya ukanda huo, huku hali ya kibinadamu ikizidi kuwa mbaya.
-
Madaktari na wauguzi wa London wataka kuachiliwa huru daktari wa watoto wa Kipalestina
Jul 13, 2026 03:08Madaktari, wauguzi na wanaharakati wamekusanyika nje ya Chuo cha Kifalme cha Watoto na Afya ya Watoto (RCPCH) jijini London, wakitaka hatua zichukuliwe dhidi ya kukamatwa kinyume cha sheria daktari wa watoto wa Kipalestina Dkt. Hussam Abu Safiya anayeshilikiwa na utawala ghasibu wa Israel.
-
Seneta Graham, msaidizi mkuu wa Trump na mchochezi mkuu wa vita dhidi ya Iran ameangamia ghafla
Jul 12, 2026 10:17Seneta Lindsey Graham, anayetambuliwa kuwa mhandisi wa mipango ya Washington dhidi ya Iran na mhamasishaji mkuu wa Trump kufanya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, hatimaye ameangamia na ndoto yake ya kunyakua "matrilioni ya dola katika pesa na mafuta ya Iran."
-
Trump amwambia Netanyahu katika malumbano makali ya simu: "Wayahudi wote wamekuchoka"
Jun 26, 2026 11:16Televisheni ya CNN ya Marekani imefichua malumbano makali ya simu baina ya Rais wa Marekani na Waziri Mkuu wa Israel ambapo Donald Trump amemkemea Benjamin Netanyahu, akimwambia: "Wayahudi wote wamekuchoka," huku Marekani ikizidisha mashinikizo kwa ajili ya kufikia makubaliano kuhusu Ukanda wa Gaza.
-
Jihad Islami yailaumu Marekani kwa ukatili unaoendelezwa na Israel huko Gaza
Jun 19, 2026 03:50Harakati ya Jihadi Islami ya Palestina imesema utawala wa Rais Donald Trump wa Marekani lazima uwajibishwe kwa ukatili na vitendo vya uchokozi vinavyofanywa na askari wa utawala vamizi wa Israel dhidi ya Wapalestina wa kawaida katika Ukanda wa Gaza ulioharibiwa na vita.
-
Wapiga picha wa Gaza washinda Tuzo ya Kalamu ya Dhahabu ya Uhuru
Jun 15, 2026 11:19Jumuiya ya Wachapishaji Habari Duniani imetangaza kwamba tuzo ya Kalamu ya Dhahabu ya Uhuru 2026 itatolewa kwa wapiga picha na wakurugenzi wa video kutoka Ukanda wa Gaza ulioharibiwa na vita.