Mahmoud Abbas aendelea kutoa vitisho dhidi ya Wapalestina wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i33204-mahmoud_abbas_aendelea_kutoa_vitisho_dhidi_ya_wapalestina_wa_gaza
Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ametishia tena kuchukua hatua kali zaidi za kuwaadhibu Wapalestina wa eneo la Ukanda wa Gaza.
(last modified 2026-03-03T12:46:59+00:00 )
Aug 16, 2017 02:49 UTC
  • Mahmoud Abbas aendelea kutoa vitisho dhidi ya Wapalestina wa Gaza

Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ametishia tena kuchukua hatua kali zaidi za kuwaadhibu Wapalestina wa eneo la Ukanda wa Gaza.

Mahmoud Abbas ametoa kitisho hicho katika mkutano na asasi na wanachama wa harakati yake ya Fat-h huko Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan na kusisitiza kuwa maadamu viongozi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina (HAMAS) hawako tayari kulegeza msimamo wao hatua za kuliadhibu eneo la Ukanda wa Gaza zitaendelezwa.

Abbas amebainisha kuwa viongozi wa Hamas wanapaswa waivunje kamati ya uendeshaji wa Gaza, waandae mazingira ya kuiwezesha serikali ya Waziri Mkuu wa Palestina Rami Hamdallah kufanya kazi zake huko Gaza na vilevile waafiki kuitishwa uchaguzi wa Bunge la Palestina.

Hali mbaya ya kibinadamu Ukanda wa Gaza

Hayo yanajiri katika hali ambayo, harakati ya Hamas ilikuwa imeshatangaza tokea hapo kabla kuwa ikiwa serikali ya Hamdallah itatekeleza mas-ulia na majukumu yote iliyonayo kuhusiana na Gaza, na serikali ya Mamlaka ya Ndani ikasimamisha hatua inazotekeleza za kuliadhibu eneo hilo, harakati hiyo itaivunja kamati hiyo ya uendeshaji.

Mamlaka ya Ndani ya Palestina inayoongozwa na Mahmoud Abbas imekuwa ikitumia mbinu tofauti kuishinikiza harakati ya Hamas ikubaliane na uamuzi wa kuitisha uchaguzi mpya wa Bunge ikiwemo kupunguza mishahara ya wafanyakazi wa Gaza, kuzuia utoaji vibali vya kuwapeleka nje ya Palestina wagonjwa wa eneo hilo, kupunguza kiwango cha mgao wa umeme unaosambazwa kwa ajili ya Wapalestina wa Gaza pamoja na kuwaachisha maelfu ya wafanyakazi wa eneo hilo.../