Al-Ahram: Muqawama wa Gaza umeiweka Israel katika fedheha na kushindwa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i49648-al_ahram_muqawama_wa_gaza_umeiweka_israel_katika_fedheha_na_kushindwa
Gazeti la Al-Ahram la nchini Misri limeandika kwamba, kurudi nyuma utawala haramu wa Kizayuni katika kukabiliana na muqawama wa eneo la Gaza, Palestina sasa kumeuweka utawala huo katika hali ya fedheha na kushindwa kijeshi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 20, 2018 23:10 UTC
  • Al-Ahram: Muqawama wa Gaza umeiweka Israel katika fedheha na kushindwa

Gazeti la Al-Ahram la nchini Misri limeandika kwamba, kurudi nyuma utawala haramu wa Kizayuni katika kukabiliana na muqawama wa eneo la Gaza, Palestina sasa kumeuweka utawala huo katika hali ya fedheha na kushindwa kijeshi.

Al-Ahram limeandika kuwa, katika siku za hivi karibuni, muqawama wa Palestina eneo la Gaza umeonyesha uwezo na nguvu zake mbele ya utawala vamizi wa Kizayuni. Katika ripoti hiyo, imeelezwa kwamba, kuvurumishwa mamia ya makombora na maroketi kutoka Ukanda wa Gaza kwenda vitongoji vya walowezi wa Kizayuni (Israel) kumezifanya fikra za walio wengi ndani ya utawala wa Kizayuni kukumbwa na wahka na wasi wasi. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, operesheni hiyo ya muqawama imeifanya Israel ishindwe kisiasa na hata kupelekea Avigdor Lieberman, Waziri wa Vita wa utawala huo ajiuzulu.

Watawala wa Kizayuni waliopatwa na fedheha kwa kushindwa na muqawama

Kadhalika gazeti la Al-Ahram limeandika kwamba, katika siku za hivi karibuni vyombo vya habari vinavyoripoti kwa lugha ya Kiebrania vya utawala wa Kizayuni pia vimekiri kwa namna tofauti kushindwa utawala huo mbele ya muqawama wa Palestina na kwamba suala hilo ni la kutisha. Wiki iliyopita wanamuqawama wa Palestina walijibu jinai za utawala haramu wa Kizayuni katika eneo la Ukanda wa Gaza, kwa kuvurumisha zaidi ya makombora 470 kwenda Israel, suala ambalo liliutia tumbojoto utawala huo khabithi.