Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni zashambulia Ukanda wa Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i54100-ndege_za_kivita_za_utawala_wa_kizayuni_zashambulia_ukanda_wa_ghaza
Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel zimewalenga Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza mapema leo Alhamisi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 13, 2019 07:25 UTC
  • Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni zashambulia Ukanda wa Ghaza

Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel zimewalenga Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza mapema leo Alhamisi.

Kwa mujibu wa taarifa, ndege za kivita za utawala wa Kizayuni zimedondosha mabomu katika eneo la kusini mwa Ukanda wa Ghaza.

Kufuatia hujuma hiyo milipuko imesikika mashariki mwa Rafah katika eneo la kusini mwa Ukanda wa Ghaza 

Jeshi la Utawala wa Kizayuni wa Israel limedai kuwa shambulizi hilo limetekelezwa baada ya maroketi kutoka Ghaza kulenga maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na utawla huo.

Katika wiki za hivi karibuni utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukitekeleza mashambulizi ya kinyama dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza kwa kutumia ndege za kivita, helikopta  na mizinga.

Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel zinalenga maeneo ya raia Ghaza

Tokea mwaka 2007, utawala haramu wa Israel umeweka mzingiro wa anga, nchi kavu na baharini dhidi ya Ukanda wa Ghaza baada ya Wapalestina katika eneo hilo kuichagua kidemokrasia harakati ya Hamas kuongoza eneo hilo. Mzingiro huo umelifanya eneo hilo lenye watu karibu milioni moja na nusu kutajwa kuwa gereza kubwa zaidi la wazi duniani.

Mbali na mzingiro huo, utawala haramu wa Israel pia umeanzisha vita mara tatu dhidi ya Ghaza tokea mwaka 2008 ambapo maelfu ya Wapalestina wakiwemo wanawake na watoto wameuawa.