Imarati na jitihada za kujinasua katika kinamasi cha vita huko Yemen
(last modified Fri, 19 Jul 2019 02:31:43 GMT )
Jul 19, 2019 02:31 UTC
  • Imarati na jitihada za kujinasua katika kinamasi cha vita huko Yemen

Msemaji wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) unajaribu kila uwezavyo ili kujinasua kwenye kinamasi cha vita huko Yemen; ambapo sasa imeebainika kuwa nchi hiyo tayari imeanza kufanya juhudi kubwa katika uwanja huo.

Msemaji wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema  Umoja wa  Falme za Kiarabu (Imarati) unajaribu kila uwezavyo ili kujinasua kwenye kinamasi cha vita huko Yemen na tayari imeanza kufanya juhudi kubwa katika uwanja huo.

Msemaji wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran ameshiria juhudi zinazofanywa na Saudia za kuzivuta nchi nyingine za Mashariki ya Kati kujiunga katika vita vya Yemen na kueleza kuwa, jitihada hizo hazijazaa matunda. Amesema kinyume chake, nchi nyingi hazijajiunga na  muungano huo na baadhi yao kama Qatar zimejitoa katika muungano huo vamizi huko Yemen na  zilizobaki zimejutia jambo hilo. 

Baadhi ya maafa ya uvamizi wa Saudia na washirika dhidi ya wananchi wa Yemen wasio na hatia
 

Sayyid Hussein Naqavi Husseini amesema kuwa vita dhidi ya watu wanaodhulumiwa wa Yemen vimeifanya Imarati ikabiliwe na vitisho chungu nzima na havijakuwa na na manufaa yoyote kwa nchi hiyo licha ya gharama zake kubwa. 

Saudia ilianzisha vita dhidi ya taifa la Yemen mwezi Machi mwaka 2015 ikiungwa mkono na Marekani, Imarati na nchi nyingine kadhaa na hadi sasa Wayemeni zaidi ya elfu 16 wameuawa, makumi ya maelfu wamejeruhiwa na mamilioni ya wengine wamekuwa wakimbizi kutokana na vita hivyo.