Waislamu waungana kupinga kuvunjiwa heshima Qur'ani huko Sweden
https://parstoday.ir/sw/news/world-i100230-waislamu_waungana_kupinga_kuvunjiwa_heshima_qur'ani_huko_sweden
Waislamu katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Iran, Iraq, Lebanon na Nigeria wamefanya maandamano makubwa na kulaani kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Sweden.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 23, 2023 09:55 UTC
  • Waislamu waungana kupinga kuvunjiwa heshima Qur'ani huko Sweden

Waislamu katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Iran, Iraq, Lebanon na Nigeria wamefanya maandamano makubwa na kulaani kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Sweden.

Katika siku 10 za karibuni vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu vimeshika kasi zaidi katika nchi za Ulaya. Sweden na Denmark, kwa mara nyngine tena, zimetoa kibali cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika nchi hizo. Kwa mara ya pili katika muda wa wiki moja, Alhamisi iliyopita wahalifu wa Sweden waliivunjia heshima Qur'ani Tukufu kwa kutumia kibali walichopewa na polisi wa nchi hiyo. Juzi Ijumaa pia kundi moja lenye misimamo ya kufuruti ada huko Denmark lilichoma moto nakala ya Qur'ani mbele ya ubalozi wa Iraq huko Copenhagen mji mkuu wa nchi hiyo.  

Kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu huko Sweden na Denmark kunaonyesha kuwa, licha ya serikali za nchi za Ulaya kudai kwamba haziungi mkono kudhalilishwa Qur'ani katika sera zao, lakini kivitendo nchi hizo zinaunga mkono na kuhamasisha vitendo hivyo vilivyo kinyume na sheria na vya kijahili. Serikali za nchi za Ulaya licha na kushuhudia namna Waislamu, katika nchi mbalimbali, walivyokasirishwa na kughadhibishwa na hujuma hizo lakini zinaandaa mazingira ya kuendelezwa vitendo hivyo badala ya kukabiliana na uhalifu huo dhidi ya matukufu ya kidini ya Waislamu zaidi ya bilioni mbili. Nchi hizo zinahalalisha vitendo vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu kwa madai ya uhuru wa kujieleza, lakini wakati huo huo zinawazuia wanafunzi wa kile Waislamu kuvaa vazi la stara la hijabu mashuleni au kuhoji na kudadisi tu madai ya Holocaust. Katika mazingira na hali kama hii, uhuru wa kujieleza huwa hauna maana yoyote. Kwa msingi huo, kuyavunjia heshima na kutangaza chuki dhidi ya matukufu ya Kiislamu katika nchi za Ulaya si uhuru wa kusema na kujieleza, bali ni hatua iliyokusudiwa na inayofanyika kwa mpangilio maalumu dhidi ya dini ya Uislamu na Waislamu.

Waislamu walaani na kupinga kuchomwa moto na kuvunjiwa heshima Qur'ani 

Hatua hii ya serikali za nchi za Ulaya na wajinga wanaoivunjia heshima Qur'ani Tukufu imekabiliwa na msimamo mkali wa Waislamu kote duniani. Baada ya kuuvamia ubalozi wa Sweden, waandamanaji waliokuwa na hasira huko Iraq wameushambulia pia ubalozi wa Denmark mjini Baghdad wakipinga uhalifu huo. Wanadiplomasia na wafanyakazi wa ubalozi wa Sweden tayari wamefukuzwa nchini Iraq. Wakati huo huo Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq imeitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za kuzuia kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na kukikaja kitendo hicho kuwa ni kiovu na cha kuchukiza. 

Wairaqi waushambulia moto Qurani huko Sweden 

Huko Lebanon na Nigeria pia wananchi wameandamana kupinga vitendo vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na kutaka kufukuzwa balozi wa Sweden katika nchi hizo. Miji mbalimbali ya Iran pia juzi Ijumaa ilishuhudia maandamano makubwa ya kulaani na kupinga kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu. Waandamananaji hao wamesisitiza kuwa, kuna ulazima wa kukabiliana na nchi zinazoruhusu vitendo hivyo vya udhalilishaji dhidi ya kitabu kitakatifu cha Waislamu.

Katika mkondo huo, Hossein Amir- Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia ametangaza kuwa: "Tehran haitampokea balozi mpya wa Sweden, na balozi mpya wa Iran hatatumwa huko Sweden." Amir- Abdollahian pia ametaka kuitishwa kikao cha dharura cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kujadili kadhia ya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika nchi za Ulaya. Saudi Arabia, Imarati na Jordan pia zimewaita mabalozi wa Sweden kwa ajili ya kujieleza.

Wakati huo huo  vyombo vya habari vya Lebanon vimetoa wito wa kufukuzwa balozi wa Sweden nchini humo. Uturuki kwa upande wake imetoa hukumu ya kukamatwa watu wanaoivunjia heshima Qur'ani Tukufu. 

Hoosein Amir- Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran 

Bila shaka, waliopata hasara kubwa katika makabiliano na Uislamu katika nchi za Ulaya ni serikali za Ulaya na Umoja wa Mataifa. Ulimwengu wa Kiislamu una suhula na uwezo mkubwa katika nyanja mbalimbali hususan katika sekta ya kiuchumi; ambapo kuongezeka pengo kati ya nchi za Kiislamu na zile za Ulaya kutazizuia nchi hizo kunufaika na suhula hizo za nchi za Kiislamu. 

Katika upande mwingine, Umoja wa Mataifa ambao aghalabu ya hati nyaraka zinazohusiana na haki za kimataifa zimepasishwa kwa usimamizi wake, haujachukua msimamo imara wa kukabiliana na vitendo vichafu vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu; kwa msingi huo nafasi ya Umoja wa Mataifa na hati hizo zitatiliwa shaka na kupoteza hadhi na heshima kutokana na msimamo wake dhaifu kuhusu suala hili.