El Niño na tishio la mafuriko Afrika Mashariki na Asia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i139862-el_niño_na_tishio_la_mafuriko_afrika_mashariki_na_asia
Shirika la Masuala ya kibinadamu limetahadharisha kuwa hali ya hewa ya El Niño inayozidi kuongezeka kwa kasi inatishia kuleta mafuriko makubwa, magonjwa na ukame katika baadhi ya jamii zilizo hatarini zaidi duniani katika eneo la Afrika Mashariki na Asia.
(last modified 2026-07-14T03:23:21+00:00 )
Jul 14, 2026 03:21 UTC
  • Tishio la El Nino Afrika Mashariki na Asia
    Tishio la El Nino Afrika Mashariki na Asia

Shirika la Masuala ya kibinadamu limetahadharisha kuwa hali ya hewa ya El Niño inayozidi kuongezeka kwa kasi inatishia kuleta mafuriko makubwa, magonjwa na ukame katika baadhi ya jamii zilizo hatarini zaidi duniani katika eneo la Afrika Mashariki na Asia.

Siku ya Jumatatu, Kamati ya Kimataifa ya Uokoaji (IRC) liliarifu kuwa Kenya, Uganda, Somalia, Bangladesh, Pakistan na Afghanistan ni miongoni mwa nchi zilizo hatarini zaidi, ambapo baadhi yake zimekuwa zikipambana na dharura za kibinadamu zinazoendelea.

"Tunashuhudia dharura kadhaa zikikutana kwa wakati mmoja, na sehemu ambazo hazina suula za kutosha ili kustahimili mshtuko mwingine ni zile zilizo katika hali ngumu," amesema Bob Kitchen, Afisa mkuu wa dharura wa Shirika la IRC.

Kituo cha Utabiri wa Hali ya Hewa cha Marekani Julai 9 mwaka huu kilieleza kuwa El Niño inaimarika kwa kasi, ikiwa na nafasi ya asilimia 81 ya kuwa moja ya matukio yenye nguvu zaidi tangu mwaka 1950, hali ambayo huenda ikafikia kilele kati ya Oktoba na Desemba mwaka huu.

Wakati huo huo huo, Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), lilitangaza mapema Julai kwamba hali ya El Niño tayari ilikuwa imeimarika na kwambahali hiyo ilitabiriwa kuimarika kwa kasi kati ya Julai na Septemba.

El Niño ni mabadiliko ya asili ya halijoto katika Bahari ya Pasifiki ambayo hujirudia kila baada ya miaka miwili hadi saba, huku pepo zinazovuma kutoka mashariki hadi magharibii kaskazini na kusini mwa Ikweta ambazo kwa kawaida husukuma maji ya uvuguvugu kuelekea magharibi zikipungua na joto huenea tena baharini.