Muhammad ni jina la pili maarufu nchini Uingereza
Jina la Mtume Mtukufu (S.A.W) ni jina la pili wanalopewa watoto wachanga nchini Uingereza huku Waislamu wakiunda asilimia sita na nusu tu ya jamii ya nchi hiyo.
Gazeti la Daily Mail limeripoti kuwa, Idara ya Takwimu ya Uingereza imetangaza kuwa jina Muhammad ni jina la pili walilopewa watoto wachanga wa kiume waliozaliwa mwaka 2022 nchini humo na huko Wales.

Miaka kumi kabla ya hapo yaani mwaka 2012 jina Muhammad liliorodheshwa kushika nafasi ya 20 miongoni mwa majina ya watoto; na 1996 jina hilo lilishika nafasi ya 180.
Kwa mujibu wa ripoti hii, jina Muhammad limeandikwa kwa njia tofauti na nafasi hii ya pili inahusiana tu na moja ya maandishi hayo huku aina nyingine za uandikaji jina Muhammad zikionekana katika jedwali la majina ya watoto wachanga waliozaliwa mwaka juzi.
Kupata umaarufu na kupendwa jina la Mtume Muhammad (S.A.W) unazidi kuongezeka katika nchi za Ulaya huku sera zilizofeli za nchi za Magharibi zikilenga kueneza chuki dhidi ya Uislamu na kuwachafua Waislamu.