Lula: Brazil haitaisahau namna Marekani ilivyosaidia kufanya mapinduzi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i129122
Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil amesema kuwa nchi yake haitasahau namna Marekani ilivyosaidia kufanya mapinduzi nchini Brazil. Rais Da Silva amelaani hatua ya Washington ya kiwekea nchi yake mashinikizo ya kisiasa na kiuchumi.
(last modified 2025-08-04T07:37:00+00:00 )
Aug 04, 2025 07:37 UTC
  • Lula: Brazil haitaisahau namna Marekani ilivyosaidia kufanya mapinduzi

Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil amesema kuwa nchi yake haitasahau namna Marekani ilivyosaidia kufanya mapinduzi nchini Brazil. Rais Da Silva amelaani hatua ya Washington ya kiwekea nchi yake mashinikizo ya kisiasa na kiuchumi.

Akizungumza katika hafla ya wafanyakazi mjini Brasilia jana Jumatatu, Rais Lula Inacio da Silva amesema kuwa Brazil haitakubali hatua za upande mmoja wa Marekani na iko tayari kutetea maslahi yake duniani. 

Rais Lula ameashiria kitisho cha karibuni cha Marekani cha kuitoza Brazil ushuru wa asilimia 50 kwa bidhaa zake zinazouzwa Marekani na kusema ni jambo lilsilokubalika kutumiwa kadhia za kisiasa kuiwekea nchi fulani vikwazo vya kiuchumi. 

" Sitasahau namna Marekani ilivyosaidia kuendesha njama ya mapinduzi" amesema Rais wa Brazil. 

Lula de Silva alisisitiza kuwa nchi yake ina uwezo wa kiuchumi na kisiasa wa kutosha kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Marekani kwa masharti sawa, lakini serikali yake italazimika kulipiza kisasi iwapo Marekani itaendelea kutumia ushuru kama njia ya kujiinua kisiasa.

Amesema nchi yake itasimama imara dhidi ya uingiliaji wowote wa nchi ajinabi. Brazili ingekabiliwa na ushuru wa kiwango cha juu iwapo Marekani ingeitoza nchi hiyo ushuru wa asilimia 50 kwa bidhaa zake zinazoingia Marekani. Trump pia alitishia kuzitoza ushuru wa ziada wa asilimia kumi nchi wanachama wa kundi la BRICS  na kuzituhumu kuwa zinajaribu kusambaratisha matumizi ya sarafu ya dola duniani.