Rais Pezeshkian: Wanawake ndio wajenzi wa nchi na mustakbali
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i134150-rais_pezeshkian_wanawake_ndio_wajenzi_wa_nchi_na_mustakbali
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kwamba haifikiriki wanawake kuwa na hadhi na thamani duni na ya chini kuliko wanaume, akisisitiza kwamba: "Wanawake ndio nguzo za jamii na wajenzi wa nchi na mustakbali wake."
(last modified 2025-12-10T11:16:28+00:00 )
Dec 10, 2025 11:16 UTC
  • Rais Masoud Pezeshkian
    Rais Masoud Pezeshkian

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kwamba haifikiriki wanawake kuwa na hadhi na thamani duni na ya chini kuliko wanaume, akisisitiza kwamba: "Wanawake ndio nguzo za jamii na wajenzi wa nchi na mustakbali wake."

Rais Masoud Pezeshkian ameyasema hayo leo Jumatano, katika sherehe ya kuadhimisha Siku ya Wanawake na Hadhi ya Akina Mama iliyofanyika katika Ukumbi Mkuu wa Mikutano mjini Tehran, akisisitiza kwamba: "Wanaume na wanawake hujenga maisha pamoja na kwa kushirikiana na wanawajibika kulea watoto na kujenga mustakabali wa nchi. Katika njia hii, mchango wa wanawake na akina mama una umuhimu na thamani kubwa, na ninaamini kwamba, ni vipofu watu ambao hawawaoni wanawake na nafasi yao ya thamani katika jamii."

Ameongeza kuwa: "Ninaamini kwamba wanawake wanaweza kuunda mustakabali wa nchi na kuwaelimisha wanaume wenye uwezo. Ninaamini kwamba moyo wa kuwa mkweli, uaminifu, na uadilifu unatoka kwa mama yangu. Kama si mama yangu, nisingekuwa hapa; hivyo hadhi na thamani ya mama yangu ni ya juu sana."

Rais Pezeshkian

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu amesema kwamba hatupaswi kufikiria kwamba thamani na hadhi ya mwanamke ni ndogo kuliko ile ya mwanaume. Amekosoa baadhi ya dhana potofu kuhusu wanawake zinazoliona tabaka hili la jamii kama wenzo tu, akibainisha kuwa: "Wanawake ndio nguzo za jamii na wajenzi wa nchi na mustakbali. Hatupaswi kupuuza nafasi hii muhimu."

Rais Pezeshkian pia amesoma Aya za Qur'ani Tukufu kuhusu imani ya haki ya mwanadamu, akiongeza: "Maisha mema huundwa kupitia imani thabiti, maarifa na kutegemea elimu na uwezo, na yanaweza kubadilisha jamii ya wanadamu."

Amesisitiza kwamba sisi sote na nafasi zetu ni wadaiwa ​​kwa mama zetu, na lazima tuwathamini na kuwaenzi akina mama na wanawake kwa juhudi zao kubwa."

Pezeshkian amehitimisha kwa kusema kwamba, uwepo wa wanawake una ufanisi katika ustawi na maendeleo ya wanaume, na kuongeza: "Natumai kwamba kupitia uwepo, juhudi na maono ya hali ya juu ya wanawake, Iran itakuwa mfano wa kuigwa katika eneo hili na dunia nzima."