Mashambulizi ya Hizbullah yalipa jeshi la kizayuni mashinikizo ambayo halijawahi kushuhudia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i137168-mashambulizi_ya_hizbullah_yalipa_jeshi_la_kizayuni_mashinikizo_ambayo_halijawahi_kushuhudia
Vyombo vya habari vya utawala wa kizayuni vimekiri kuwa jeshi la utawala huo ghasibu liko kwenye mashinikizo ambayo halijawahi kushuhudia kutokana na mashambulio ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon kwenye medani ya kaskazini ya vita ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
(last modified 2026-03-05T04:28:24+00:00 )
Mar 05, 2026 04:28 UTC
  • Mashambulizi ya Hizbullah yalipa jeshi la kizayuni mashinikizo ambayo halijawahi kushuhudia

Vyombo vya habari vya utawala wa kizayuni vimekiri kuwa jeshi la utawala huo ghasibu liko kwenye mashinikizo ambayo halijawahi kushuhudia kutokana na mashambulio ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon kwenye medani ya kaskazini ya vita ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Duru za habari za Palestina zimetangaza kuwa, Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon unaendelea kufanya mashambulio makali na yenye wigo mpana dhidi ya wanajeshi wa kizayuni na vitongoji haramu vya walowezi katika mpaka wa pamoja wa Lebanon na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu zilizopachikwa jina bandia la Israel.

Kamandi ya jeshi la utawala wa kizayuni katika eneo la kaskazini alfajiri ya kuamkia leo Alkhamisi imewaamuru walowezi wa kizayuni wanaoishi vitongoji haramu 22 vya mpakani wasalie kwenye maficho au sehemu zingine zenye usalama.

Wakati huohuo, vyombo vya habari vya utawala wa kizayuni vimeripoti kuwa, wanajeshi za kizayuni wamefikwa na tukio kubwa katika eneo la kusini mwa Lebanon.

Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa shambulio la Muqawama limelenga moja kwa moja kifaru au gari ndogo ya kijeshi ya utawala wa kizayuni kwenye mpaka wa Lebanon…/