Hujjatul-Islam Qommi: Mchakato wa kumchagua Kiongozi Mkuu mpya unakaribia kukamilika
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137176-hujjatul_islam_qommi_mchakato_wa_kumchagua_kiongozi_mkuu_mpya_unakaribia_kukamilika
Mjumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Wanazuoni Wataalamu linalomchagua Kiongozi Mkuu amesema, mchakato wa kumchagua Kiongozi Mkuu mpya unakaribia kukamilika.
(last modified 2026-03-05T06:02:34+00:00 )
Mar 05, 2026 06:02 UTC
  • Hujjatul-Islam Qommi: Mchakato wa kumchagua Kiongozi Mkuu mpya unakaribia kukamilika

Mjumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Wanazuoni Wataalamu linalomchagua Kiongozi Mkuu amesema, mchakato wa kumchagua Kiongozi Mkuu mpya unakaribia kukamilika.

Hujjatul-Islam Wal-Muslimin Mohsen Qommi ameeleza hayo katika mahojiano na televisheni ya hapa nchini na kufafanua kuwa, mchakato wa kumchagua Kiongozi Mkuu mpya kwa mujibu wa misingi ya Katiba na kanuni zilizomo kwenye muongozo wa ndani wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu unakaribia kukamilika, na kwamba tetesi zinazoenezwa kwenye mitandao ya kijamii hazina mashiko ya kisheria.

Mjumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Wanazuoni Wataalamu amekumbusha kuwa, baraza hilo la kumchagua Kiongozi Mkuu hivi sasa linatekeleza jukumu lililokabidhiwa ili kuweza kumtangaza haraka iwezekanavyo Kiongozi Mkuu mpya kwa mujibu wa Msingi wa 11 wa Katiba.

Hujjatul-Islam Qommi amesisitiza kuwa, wananchi wasishughulishwe na uvumi, na kwamba taarifa wanazohitajia wazifuatilie kupitia kamati ya uongozi tu ya Baraza la Wanazuoni Wataalamu…/