Mauzo ya chai ya Iran nje ya nchi yaongezeka kwa 48%
Mkuu wa Shirika la Chai la Iran, Habib Jahansaz amesema mauzo ya chai ya Jamhuri ya Kiislamu nje ya nchi katika miezi minane ya kwanza ya mwaka huu wa kalenda ya Iran (ulioanza Machi 21) yameongezeka kwa asilimia 48, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Takriban tani milioni 9.8 za chai bora ya Iran zilisafirishwa hadi kwenye masoko lengwa ya nje kati ya Machi 21 na Novemba 22, 2025, amesema.
Akifafanua hatua za hivi karibuni zilizochukuliwa na shirika lake, Jahansaz amesisitiza kuwa, "Kwa ufuatiliaji usiokoma, hatua madhubuti zilichukuliwa ili kuwasaidia wakulima wa chai nchini."
Iran ilisafirisha chai bora yenye thamani ya dola milioni 12 hadi kwenye masoko ya kigeni kati ya Machi 21 na Novemba 22, 2025, amefafanua afisa huyo wa Iran.
Mkuu wa Shirika la Chai la Iran ameeleza bayana kuwa, hatua madhubuti zimechukuliwa ili kupunguza uagizaji wa chai nchini.
"Uzalishaji wa ndani wa chai yenye vifurushi mbalimbali ikiwa ni pamoja na chai ya kijani na chai ya mimea unaweza kuongeza sehemu ya mauzo ya nje ya Iran katika soko la kimataifa," Jahansaz ameongeza.