-
Leo Ijumaa, wananchi wa Iran wanashiriki katika uchaguzi wa Bunge na Baraza la Wanazuoni Wataalamu
Feb 21, 2020 03:05Uchaguzi wa Bunge la 11 la Iran linalojulikana kwa jina la Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu na uchaguzi wa kwanza mdogo wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu wanaomchagua na kusimamia kazi za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, unafanyika leo Ijumaa kuanzia saa mbili asubuhi katika kona zote za Iran.
-
Iran: Kwa mara nyingine Marekani imedhihirisha udhalili wake
Apr 16, 2019 06:58Msemaji wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, hatua ya Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya ya kuzuia kutumwa misaada ya nchi nyingine kwa ajili ya wahanga wa mafuriko nchini Iran, imedhihirisha udhalili wake wa kukabiliana na ubinaadamu na haki za msingi za kibinaadamu.
-
Kiongozi Muadhamu asisitizia umuhimu wa kukabiliana na hujuma kubwa ya maadui wa Iran
Mar 14, 2019 14:26Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, katika kukabiliana na hujuma kubwa za maadui ni lazima kuchukuliwe hatua za kujitolea kukubwa kwa nyenzo, uwezo na watu ili kuthibitisha kivitendo imani ya wananchi na viongozi juu ya kukumbuka na kumtegemea Mwenyezi Mungu na kwamba ahadi za Mwenyezi Mungu kuhusu taifa kubwa la Iran zinatimia.
-
Kiongozi: Lengo la adui katika vita vya vyombo vya habari ni kuwafadhaisha na kuwakatisha tamaa wananchi
Sep 06, 2018 14:49Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyed Ali Khamenei amesema, jukumu muhimu zaidi walilonalo wananchi na wenye vipawa katika hali nyeti na hasasi ya hivi sasa ni kupiga hatua mbele katika kudumisha na kuimarisha mshikamano baina ya wananchi na vyombo vya serikali na kujiepusha na kujenga mazingira ya kupoteza matumaini na kukatisha tamaa na kuhisi kwamba kuna mkwamo.
-
Ayatullah Jannati: Kujiondoa Marekani katika mapatano ya nyuklia ya Iran liwe funzo
Sep 04, 2018 13:32Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ahamad Jannati ameashiria Marekani kuvunja ahadi zake na kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya Iran, JCPOA, na kusema hilo linapaswa kuwa funzo kuhusu mazungumzo na Marekani.
-
Kiongozi Muadhamu: Imani na ucha-Mungu, ni sababu ya kusimama imara taifa la Iran dhidi ya hujuma za Marekani na Israel
Mar 15, 2018 14:55Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kusimama imara na mafanikio ya Iran katika kukabiliana na hujuma za mrengo mkubwa wa kisiasa, kifedha, kijeshi, kiusalama na kiutamaduni wa Marekani na Israel, kunatokana na baraka za kuwepo imani na ucha-Mungu baina ya matabaka ya wananchi na vijana wa Iran.
-
Iran imebadilisha changamoto, vitisho kuwa fursa zisizo na kifani
Mar 14, 2018 02:45Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema changamoto na vitisho vyote vya kigeni dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran vimebadilishwa na kuwa fursa zisizo na kifani.
-
Kiongozi Muadhamu: Malengo ya Mapinduzi yatafikiwa kwa kutekeleza 'Jihadi Kubwa' ya kutomtii adui
May 26, 2016 16:37Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema njia pekee ya kuufanya Mfumo wa Kiislamu udumu na kupiga hatua mbele na kufikiwa malengo ya Mapinduzi ni 'nchi kuwa na uwezo halisi' na kutekelezwa 'jihadi kubwa', yaani kutomtii adui.
-
Baraza la Tano la Wanazuoni wa Kumchagua Kiongozi lazinduliwa kwa ujumbe wa Kiongozi Muadhamu
May 24, 2016 16:23Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema jukumu la Baraza la Wanazuoni Wataalamu wa Kumchagua Kiongozi Mkuu ni kulinda kwa umakini na kwa hali zote utambulisho wa Kiislamu na Kimapinduzi wa Mfumo.