Barabara ya Hariri ya Kusini: Iran, Uturuki zarekebisha biashara ya Eurasia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i134110-barabara_ya_hariri_ya_kusini_iran_uturuki_zarekebisha_biashara_ya_eurasia
Mwishoni mwa mwezi uliopita, wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan alipofanya ziara mjini Tehran, Iran na Uturuki zilitangaza makubaliano ya kuanza ujenzi wa njia mpya ya pamoja ya reli kati ya nchi mbili.
(last modified 2025-12-09T15:23:13+00:00 )
Dec 09, 2025 11:31 UTC
  • Barabara ya Hariri; Iran na Uturuki
    Barabara ya Hariri; Iran na Uturuki

Mwishoni mwa mwezi uliopita, wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan alipofanya ziara mjini Tehran, Iran na Uturuki zilitangaza makubaliano ya kuanza ujenzi wa njia mpya ya pamoja ya reli kati ya nchi mbili.

Maafisa wa Iran na Uturuki wameutaja mradi huo kama hatua ya kipaumbele kuelekea kuunganisha mpakani reli za nchi hizo mbili  na kuendeleza ukanda wa biashara wa kimkakati unaounganisha Asia na Ulaya.

Makubaliano hayo yanajumuisha kuanza  kazi kwenye njia ya usafiri ya Marand-Cheshmeh Soraya yenye takriban kilomita 200 ambayo itafika hadi katika eneo la mpaka w Uturuki wa Aralık.

Takwimu zilizotolewa na maafisa wa Iran zinaonyesha kuwa, mradi huo una thamani ya takriban dola bilioni 1.6 na umepangwa kukamilika ndani ya miaka mitatu hadi minne.

Njia hii mpya ya reli ni ishara ya wazi  kwamba nchi zilizo kwenye njia hii zimeazimia kubadilisha jiografia kuwa chachu ya maendeleo..

Njia hiyo mpya ya reli ya pamoja kati ya Iran na Uturuki  ili kuunganisha pamoja mhimili wa Marand-Maku- Bazargan kuelekea mashariki mwa Uturuki. Mradi huo unajaza pengo la kimuundo kati ya mitandao miwili mikubwa ya reli ya eneo hilo. 

Marhala nyingine ya mradi huo, kuhuisha huduma ya reli ya Istanbul-Tehran-Islamabad (ITI), iliyopangwa kufunguliwa tena Januari 2026.