Jibu la watumiaji wa mtandao wa X kwa tishio la shambulio la nchi kavu la Marekani: Tunawasubiri, njooni, majeneza yako tayari!
-
Wairani wawaambia wanajeshi wa Marekani: Tutakuzikeni hapa hapa, majeneza yako tayari
Watumiaji wa mtandao wa kijamii wa X wamevitaja vitisho vya Marekani vya kuanzisha mashambulizi na uvamizi wa nchi kavu dhidi ya Iran kuwa ni dhihirisho lingine la kukata tamaa kwa Marekani dhidi ya nguvu ya kijeshi na ulinzi ya Iran.
Wanaharakati wa Iran katika mtandao wa X wamesisitiza kwamba wanasubiri kwa hamu kubwa kuwapa somo wavamizi wa Kimarekani.
Mwanaharakati wa Iran, Reza Abbasi ameandika: "Aina bora ya vita kwetu ni ile ya nchi kavu, kwa sababu tuna utaalamu wa kilinda ardhi yetu dhidi ya adui. Tutaifanya Iran kuwa makaburi ya Wamarekani. Mtaona kitakachotokea."
Davud Modarresian amesema: "Nguvu ya Marekani ni nguvu yake ya anga na majini, ambayo haijaweza kufanya lolote hadi sasa. Katika vita vya anga na makombora, Iran imeweza kuharibu kambi za Marekani katika eneo la Asia Magharibi na kuwafanya makamanda na wanajeshi wake wakimbie. Sasa Marekani inataka kukabiliana nasi katika vita vya nchi kavu? Karibu, tunasubiri."
Kwa upande wake, Fatima amesisitiza: "Shambulio la nchi kavu dhidi ya Iran lina maana ya kuandaa majeneza zaidi kwa ajili ya wanajeshi wa Marekani."
Mtumiaji wa mtandao wa X aliyejitambulisha kwa jina la ‘Raha" pia amewaambia Wamarekani: "Njozi ya shambulio la nchi kavu itakuwa kosa lenu la mwisho. Historia ni uthibitisho kwamba ardhi ya Iran ni makaburi ya wavamizi. Tutakuzikeni hapa hapa."
Hami, anaamini: "Maseneta walioota kushambulia Iran bado hawajatambua nguvu ya ulinzi na utashi wa taifa la Iran. Usalama wetu hauwezi kuyumbishwa na wacheza kamari ya kisiasa nchini Marekani."
Poriya ameandika: "Someni historia ili muone Wairani walichowafanyia wavamizi wa Kiingereza na Kireno katika ardhi ya nchi hii."