Muigizaji wa Marekani: Trump anastahili kuwa gerezani sio White House
https://parstoday.ir/sw/news/world-i137838-muigizaji_wa_marekani_trump_anastahili_kuwa_gerezani_sio_white_house
Muigizaji mmoja wa Marekani amesema kwamba rais wa nchi hiyo, Donald Trump, anastahili kufungwa jela na siyo kuwa White House.
(last modified 2026-04-13T11:58:29+00:00 )
Apr 12, 2026 09:47 UTC
  • Mark Ruffalo
    Mark Ruffalo

Muigizaji mmoja wa Marekani amesema kwamba rais wa nchi hiyo, Donald Trump, anastahili kufungwa jela na siyo kuwa White House.

Muigizaji wa Hollywood, Mark Ruffalo, amejibu vitisho vya hivi karibuni vya Rais wa Marekani, Donald Trump dhidi ya Iran kwamba "ataua ustaarabu mzima wa Iran," na kusema: "Trump ni mwendawazimu wa mauaji ya kimbari. Anapaswa kuwekwa jela kwa kutumia lugha isiyofaa na ya kuitishia Iran."

"Lugha anayotumia inaishia moja kwa moja kwenye mauaji ya kimbari," ameongeza Ruffalo na kusema: "Hii ndiyo lugha ileile iliyosababisha mauaji ya kimbari huko Gaza, janga ambalo Marekani ilisaidia sana kufanyika kwake, na sasa tuna rais ambaye anakariri lugha hiyo hiyo."

Kwa upande wake, mchambuzi maarufu wa Marekani, Tucker Carlson ameendelea kumkosoa rais wa nchi hiyo na kusema kwamba Donald Trump anaweza kukabiliwa na "mashinikizo" kutoka Tel Aviv katika juhudi za kukomesha vita dhidi ya Iran. Carlson ameongeza: "Vyombo vya habari vyenye mfungamano na serikali ya Washington haviripoti kamwe suala hili, lakini Tel Aviv ina historia ndefu ya kuwatishia marais wa Marekani."

Tucker Carlson ameendelea kusema: "Historia ya Israel inaonyesha kwamba viongozi wake wako tayari kutumia mashinikizo kadiri inavyowezekana ili kuendeleza umwagaji damu."