Umoja wa Ulaya watakiwa kusitisha ushirikiano wake na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/world-i129500-umoja_wa_ulaya_watakiwa_kusitisha_ushirikiano_wake_na_israel
Umoja wa Ulaya umetakiwa usitishe ushirikiano wake na utawala wa kizayuni wa Israel kutokana na jinai za utawala huo ghasibu dhidi ya Wapalestina hususan katika Ukanda wa Gaza.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Aug 14, 2025 00:08 UTC
  • Makao makuu yya UUmoja wa Ulaya mjini Brussels Ubelgiji
    Makao makuu yya UUmoja wa Ulaya mjini Brussels Ubelgiji

Umoja wa Ulaya umetakiwa usitishe ushirikiano wake na utawala wa kizayuni wa Israel kutokana na jinai za utawala huo ghasibu dhidi ya Wapalestina hususan katika Ukanda wa Gaza.

Mkuu wa zamani wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell pamoja na zaidi ya wabunge 110 wa zamani wa Bunge la Ulaya wametoa wito wa kusitishwa Makubaliano ya Ushirikiano na Ushirika kati ya Umoja wa Ulaya na utawala wa Israel. Katika taarifa yao, Borrell na zaidi ya wabunge 110 wa zamani wa Bunge la Ulaya wameonya katika taarifa yao kwamba kushindwa kuchukua hatua kutauweka Umoja wa Ulaya katika hatari ya kukiuka Kifungu cha 265 cha Mkataba wa umoja huo kutokana na "uzembe wa makusudi."

Tovuti ya Observer wa Umoja wa Ulaya hapo awali uliripoti kwamba, mawakili wa Ufaransa na Ubelgiji wanatarajiwa kuwasilisha malalamiko ya kushindwa katika Mahakama ya Haki ya Umoja wa Ulaya huko Luxembourg ya kushindwa Tume na Baraza la Ulaya a kuchukua hatua dhidi ya uhalifu uliofanywa na utawala wa Israel iliyofanya uvamizi katika Ukanda wa Gaza na kulikalia kwa mabavu eneo.

Tovuti hiyo imeongeza kuwa, malalamiko hayo ambayo yatawasilishwa dhidi ya Tume ya Umoja wa Ulaya na Baraza la Ulaya yanatokana na Kifungu cha 265 cha Mkataba wa Umoja wa Ulaya, ambacho kinalenga kuiadhibu taasisi yoyote ya Ulaya kwa kushindwa kuchukua hatua.

Malalamiko hayo yametokana na kushindwa kwa Kamisheni ya Ulaya na Baraza la Ulaya kusitisha makubaliano ya ushirikiano na utawala wa Kizayuni kwa muda wa miezi 21 (kuanzia Oktoba 2023), sambamba na kushindwa kupendekeza vikwazo vyovyote au vikwazo vya kiuchumi dhidi ya baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu na kushindwa kuchukua misimamo ya umma kuhusu hatari ya mauaji ya kimbari na uhalifu wenye ushahidi na nyaraka za kutosha.