Umoja wa Mataifa: Unyanyasaji kijinsia katika maeneo ya mizozo uliongezeka 2024
https://parstoday.ir/sw/news/world-i129576-umoja_wa_mataifa_unyanyasaji_kijinsia_katika_maeneo_ya_mizozo_uliongezeka_2024
Umoja wa Mataifa umetangaza katika ripoti iliyotolewa yake kwamba, vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo yenye migogoro kote duniani viliongezeka kwa asilimia 25 mwaka jana (2024).
(last modified 2025-08-15T22:50:15+00:00 )
Aug 15, 2025 22:50 UTC
  • Umoja wa Mataifa: Unyanyasaji kijinsia katika maeneo ya mizozo uliongezeka 2024

Umoja wa Mataifa umetangaza katika ripoti iliyotolewa yake kwamba, vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo yenye migogoro kote duniani viliongezeka kwa asilimia 25 mwaka jana (2024).

Kwa mujibu wa ripoti hiyo idadi kubwa ya visa vya unyanyasaji wa kijinsia viliiripotiwa katika nchi za Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kongo, Haiti, Somalia na Sudan Kusini.

Ripoti ya kila mwaka ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ilisema zaidi ya watu 4,600 walinusurika unyanyasaji wa kijinsia mwaka 2024, huku makundi yenye silaha yakifanya unyanyasaji mwingi lakini pia na vikosi vya serikali.

Ripoti hiyo inavitaja vyama 63 vya serikali na visivyo vya kiserikali katika nchi kadhaa vinavyoshukiwa kufanya au kuhusika na ubakaji na aina nyingine za unyanyasaji wa kingono katika mzozo.

Unyanyasaji wa kingono na mateso kwa kina mama na wasichana kupewa mimba za kulazimishwa yalifanyika wakati na baada ya vita katika eneo la Tigray nchini Ethiopia.

Maandamano ya kupinga ubakaji nchini India

 

Mashirika mawili yasiyo ya kiserikali ya kutetea haki za binadamu yameeleza katika ripoti yao inayojumuisha "uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu."

Mwanzoni mwa mwaka huu, Umoja wa Mataifa ulizishutumu pande mbili za vita vya wenyewe kwa wenyewe katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa zinahusika na mauaji ya watu wengi na ubakaji.

Aidha serikali ya Sudan ilitangaza Januari mwaka huu kwamba, zaidi ya wanawake 500 wamebakwa na wanamgambo wa Sudan tangu kuanza kwa vita dhidi ya jeshi mnamo mwezi Aprili 2023.