Uhispania: Mikataba yote na Israel inapaswa kusitishwa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i129596-uhispania_mikataba_yote_na_israel_inapaswa_kusitishwa
Naibu Waziri Mkuu wa Uhispania amesisitiza ulazima wa kusitishwa mikataba yote na kusimamisha biashara na utawala wa Kizayuni ili kukabiliana na "uchumi wa mauaji ya kimbari."
(last modified 2025-08-16T07:27:58+00:00 )
Aug 16, 2025 03:34 UTC
  • Yolanda Diaz, Naibu Waziri Mkuu wa Pili wa Uhispania na Waziri wa Kazi na Uchumi wa Kijamii,
    Yolanda Diaz, Naibu Waziri Mkuu wa Pili wa Uhispania na Waziri wa Kazi na Uchumi wa Kijamii,

Naibu Waziri Mkuu wa Uhispania amesisitiza ulazima wa kusitishwa mikataba yote na kusimamisha biashara na utawala wa Kizayuni ili kukabiliana na "uchumi wa mauaji ya kimbari."

Yolanda Diaz, Naibu Waziri Mkuu wa Pili wa Uhispania na Waziri wa Kazi na Uchumi wa Kijamii, amesema katika taarifa yake kabla ya kushiriki katika maandamano ya kuunga mkono Palestina yaliyofanyika katika eneo la Praia America la Galicia, Uhispania: "Kudumisha uhusiano wa kibiashara na makampuni ya Israel ni kuendeleza mauaji ya halaiki huko Palestina, na Umoja wa Ulaya pia lazima usitishe mikataba ya silaha na Israel."

Amesisitiza kuwa kinachoendelea Palestina kwa kuzingatia “kukaliwa kwa mabavu kikamilifu Gaza na ukiukaji wa moja kwa moja wa sheria za kimataifa" ni "kikubwa kabisa.

Maandamano ya kutaka kutengwa Israel kutokana na jinai zake dhidi ya wakazi wa Gaza

 

Naibu Waziri Mkuu wa Pili wa Uhispania na Waziri wa Kazi na Uchumi wa Kijamii  amesema pia kuwa,"Wagaza wanaendelea  na njaa inatumiwa kama mkakati wa vita. "Tunachokiona hakivumiliki na ndiyo maana ni lazima tuitake jamii ya kimataifa kufanya kile ambacho serikali ya Uhispania inafanya. Mauaji haya ya kimbari lazima yakome."

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania José Manuel Álvarez hivi karibuni alitangaza kuongezeka kwa shinikizo kwa Umoja wa Ulaya na ombi la Madrid la kusimamisha "Makubaliano ya Ushirikiano na Israel," akisisitiza haja ya kuchukuliwa hatua za adhabu dhidi ya utawala wa Kizayuni ili kuhakikisha unakomesha  mashambulizi ya kijeshi huko Gaza na kusema kwamba "hadhi na itibari ya Ulaya iko hatarini.