Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa: Ni wakati wa kuchukua hatua; tunahitaji usitishaji mapigano mara moja Gaza
https://parstoday.ir/sw/radio/daily_news-i129946-katibu_mkuu_wa_umoja_wa_mataifa_ni_wakati_wa_kuchukua_hatua_tunahitaji_usitishaji_mapigano_mara_moja_gaza
Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema kuhusiana na tangazo rasmi la mgogoro wa baa la njaa huko Gaza, kwamba anaamini kuwa sasa ni wakati wa kuchukuliwa hatua na kwamba usitishaji mapigano unapasa kutekelezwa mara moja na misaada ya kibinadamu kuruhusiwa kuingia katika ukanda huo bila masharti wala vikwazo vyovyote.
(last modified 2025-08-24T12:09:21+00:00 )
Aug 24, 2025 12:02 UTC
  • Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa: Ni wakati wa kuchukua hatua; tunahitaji usitishaji mapigano mara moja Gaza

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema kuhusiana na tangazo rasmi la mgogoro wa baa la njaa huko Gaza, kwamba anaamini kuwa sasa ni wakati wa kuchukuliwa hatua na kwamba usitishaji mapigano unapasa kutekelezwa mara moja na misaada ya kibinadamu kuruhusiwa kuingia katika ukanda huo bila masharti wala vikwazo vyovyote.

Danny Ylagros, Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anaamini kwamba wakati ambapo inaonekana kwamba hakuna maneno yaliyosalia ya kubainisha Jahanna hai ya Gaza, neno jipya limeongezwa; baa la njaa kali. Msemaji huyu wa Umoja wa Mataifa ameongeza: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anasema kwamba hatuwezi kuruhusu hali hii iendelee bila kuadhibiwa wahusika. Hakuna visingizio tena na wakati wa kuchukua hatua sio kesho, ni sasa hivi. Tunahitaji usitishaji mapigano mara moja, kuachiliwa mara moja kwa mateka wote na ufikiaji kamili na usio na kikomo wa misaada ya kibinadamu.