Jumamosi, 15 Februari, 2025
Leo ni Jumamosi 16 Shaaban 1446 Hijria mwafaka na 15 Februari 2025 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 243 iliyopita sawa na tarehe 15 Februari 1782 vilianza vita vya majini kati ya Ufaransa na Uingereza katika pwani ya India. Vita hivyo vilivyodumu kwa muda wa miezi saba, vilikuwa ni mlolongo wa vita kati ya nchi mbili hizo vilivyokuwa na lengo la kuikoloni India na kupora utajiri wake. Ijapokuwa Ufaransa ilishinda vita hivyo, lakini nchi hiyo haikuweza kurejea India na kuikoloni nchi hiyo, na badala yake Uingereza ilibaki na kuendelea kuwa mkoloni mkuu huko Bara Hindi.

Katika siku kama ya leo miaka 164 iliyopita, Alfred North Whitehead mwanahisabati mahiri wa Uingereza alizaliwa. Baada ya kukamilisha masomo yake alianza kufundisha falsafa na hisabati katika vyuo vikuu vya Marekani na Uingereza. Alfred North Whitehead ameandikka pia vitabu kuhusiana na hisabati. Tofauti na ilivyo9kkuwa katikka zama zake za ujana ambapo alikuwa na mapenzi makubwa na hisabati, katika miaka ya mwisho wa umri wake aliondokea kkuwa na mapenzi na falsafa. Kutokana na kuwa Alfred North Whitehead alikuwa kkatika familia ya kidini, alikuwa akitoa umuhimu upande wa kimaanawi wa dunia kulikko upande wa kimaada.

Miaka 71 iliyopita katika siku kama ya leo kulingana na kalenda ya Hijria Shamsia, Aliaga dunia Ayatullah Sheikh Abdul-Hussein Rashti, fakihi na mwanafalsafa wa Kiirani. Alizaliwa mwaka 1292 Hijria katika mji wa Karbala, Iraq. Akiwa pamoja na baba yake alielekea Rasht Iran akkiwa bado kijana mdogo na kusoma masomo ya msingi na ya kati katika mji huo. Aidha akiwa na umri wa miaka 20 Abdul-Hussein Rashti alielekea Tehran na kuhudhuria masomo na darsa za wanazuoni wakubwa katika zzama hizo kkama Sheikh Muhammad Hassan Ashtiyani, Sheikh Ali Nuri, Sayyid Shahab al-Din Tabrizi Shirazi na Mirza Abul-Hassan.

Miaka 46 iliyopita katika siku kama ya leo ya tarehe 27 Bahman, idadi kadhaa ya viongozi wa utawala wa Kipahlavi walinyongwa baada ya kupatikana na hatia ya usaliti na kutenda jinai dhidi ya wananchi wa Iran. Licha ya kuwa kwa mtazamo wa wananchi Waislamu wa Iran jinai za viongozi hao wa utawala dhalimu wa Shah zilikuwa wazi na bayana, lakini kwa amri ya Imam Khomeini MA mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu kuliundwa Mahakama ya Mapinduzi ya Kiislamu na kushughulikia kesi za viongozi hao waliokuwa wametiwa mbaroni na vikosi vya wananchi. Katika kesi ya kwanza, makamanda wanne wa jeshi ambao walikuwa na mchango mkubwa katika mauaji dhidi ya raia walihukumiwa kunyonga. Mmoja wa watu hao alikuwa Nematollah Nasiri, Mkuu wa Shirika la Intelijensia na Usalama la Shah lililokuwa maarufu kama SAVAK, ambye alikuwa mkuu wa shirika hilo la kuogofya kwa zaidi ya miaka 13 ambapo katikak kipindi ckae cha uongozi aliwatia mbaroni maelefu ya wanamapambano wa kiislamu, kuwatesa na kuwaua wengi miongoni mwao.

Miaka 36 iliyopita katika siku kama ya leo Jeshi Jekundu la Shirikisho la Urusi ya zamani lililazimika kuondoka nchini Afghanistan baada ya kuikalia kwa mabavu nchi hiyo kwa miaka kumi. Majeshi hayo yaliondoka baada ya kushindwa kukabiliana na muqawama wa mujahidina wa Kiislamu. Lengo la Umoja wa Sovieti la kuivamia na kuikalia kwa mabavu Afghanistan mwaka 1979, lilikuwa ni kuizatiti na kuitia nguvu serikali kibaraka ya Kabul iliyokuwa ikiungwa mkono na Moscow na kueneza satua yake upande wa maeneo ya kusini mwa Asia. Hatua hiyo iliyoyatumbukiza hatarini maslahi ya Marekani, ilikabiliwa na radiamali kali ya Washington ambapo Ikulu ya Marekani (White House) ilianzisha operesheni za kuyatoa majeshi ya Umoja wa Sovieti huko Afghanistan. Hatimaye baada ya miaka 10 wananchi wa Afghanistan wakisaidiwa na Mujahidina walifanikiwa kuhitimisha uvamizi huo na kuyatoa majeshi ya Urusi katika ardhi yao.
