Sep 24, 2025 02:17 UTC
  • Jumatano 24 Septemba

Leo ni Jumatano tarehe Mosi Rabiul Thani 1447 Hijria Qamaria sawa na Pili Mehr mwaka 1404 Hijria Shamsia, inayosadifiana na tarehe 24 Septemba 2025 Miladia.

Miaka 382 iliyopita katika siku kama ya leo, tarehe 24 Septemba mwaka wa 1643 Miladia:

Scotland iliunganishwa rasmi na Uingereza. Scotland iko katika sehemu ya kaskazini ya kisiwa cha Uingereza, eneo lenye milima, misitu minene, na malisho mapana, likitenganishwa na ardhi kuu ya Uingereza kwa mito kadhaa na ghuba ya Solway. Tangu zama za kale, eneo hili lilikuwa na makaazi ya watu, na baadaye likawa makazi ya baadhi ya makabila kutoka Uingereza. Katika karne zilizofuata, lugha na tamaduni za Kiingereza ziliendelea kupenya katika maeneo haya.

Hata hivyo, hali ya vita na amani kati ya Scotland na Uingereza iliendelea kwa muda mrefu. Mwanzoni mwa karne ya kumi na saba, mazingira ya kuleta umoja kati ya maeneo haya mawili yalianza kuundwa, hadi hatimaye mnamo tarehe 24 Septemba 1643, muungano wa kisiasa na mshikamano wa kitaifa kati ya Scotland na Uingereza ulitekelezwa rasmi.

 

Miaka 125 iliyopita, katika siku kama ya leo—tarehe 1 Rabi' al-Thani mwaka 1322 Hijria:

Mulla Ali bin Fathullah Nahavandi, mmoja wa maulamaa wakubwa wa madhehebu ya Shia, aliyekuwa akiishi Najaf, Iraq alifariki dunia. Mulla Ali bin Fathullah Nahavandi Najafi alikuwa miongoni mwa wasomi mashuhuri wa zama zake, na ni miongoni mwa wanafunzi wa Sheikh Murtadha Ansari na Mirza Abul-Qasim Kalantari.

Miongoni mwa kazi zake za kielimu ni Tashrih al-Usul al-Saghir na Muqaddimat al-Wajib, ambazo zinaendelea kuthaminiwa katika muktadha wa elimu ya fiqh na usul. Kifo chake kilitokana na maradhi ya kipindupindu, na mwili wake ulizikwa katika makaburi ya Wadi al-Salaam huko Najaf, mahali patakatifu pa mapumziko ya maulamaa na waumini.

Katika siku kama ya leo miaka 86 iliyopita, ndege za kijeshi za Ujerumani zilianza kufanya mashambulio makubwa dhidi ya mji mkuu wa Poland, Warsaw.

Mashambulio hayo yalifanyika sambamba na kuanza Vita Vikuu vya Pili vya Dunia na yaliendelea kwa muda wa siku tatu. Hatimaye wananchi wa mji huo walisalimu amri mbele ya majeshi ya Ujerumani baada ya mapambano na siku kumi na moja.

Mashambulio hayo ya kinyama yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 15,000.

 

Katika siku kama ya leo miaka 51 iliyopita, Guinea Bissau ilitangaza uhuru wake kutoka kwa mkoloni Mreno.

Guinea Bissau iligunduliwa mwaka 1446 na Mwana Mfalme Henry aliyekuwa akitawala Ureno pamoja na wenzake na kuwa koloni la nchi hiyo. Guinea Bissau ambayo ilikuwa ikijulikana kwa jina la Guinea Ureno, ilikuwa miongoni mwa vituo vya biashara ya utumwa ya wazungu katika karne za 17 na 18.

Na hatimaye ilipofika mwaka 1974, Ureno ikakubali kuwa huru nchi ya Guinea Bissau. Guinea Bissau iko kaskazini magharibi mwa Afrika na katika pwani ya Bahari ya Atlantic. 

 

Miaka mitatu iliyopita katika siku kama ya leo, tarehe 2 Mehr mwaka 1402 Hijria Shamsiya

Amin Tarokh, msanii maarufu wa Iran, alifariki dunia. Alizaliwa tarehe 20 Mordad mwaka 1332 Hijria Shamsiya katika mji wa Shiraz, na baada ya kufanikiwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Tehran mnamo mwaka 1351, alihamia Tehran. Baada ya kuhitimu katika taaluma ya sanaa ya maonyesho, alianza kushiriki katika maigizo ya jukwaani, filamu za sinema na vipindi vya televisheni.

Umaarufu wake ulianza kwa kushiriki katika kipindi maarufu cha televisheni  cha Sarbedaran katika miaka ya 1360 Hijria. Baadaye alikuwa muigizaji katika kazi vipindi vingi  mashuhuri kama vile Abu Ali Sina, Delshodegan, Parandeh-ye Kuchak-e Khoshbakhti, Sarb, Madar, Sheikh Mofid na vinginevyo.Katika kipindi cha kazi yake ya uigizaji, alitunukiwa tuzo mbalimbali za kitaifa na kimataifa.

Msanii huyu mwenye bidii na mwenye kupendwa sana na watu wa Iran, hatimaye alilazwa hospitalini katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) mnamo tarehe 28 Shahrivar kutokana na mshtuko wa moyo. Kwa masikitiko makubwa, alifariki dunia siku nne baadaye, tarehe 2 Mehr 1401, akiwa na umri wa miaka 69.