Oct 08, 2025 02:39 UTC
  • Jumatano, 08 Oktoba 2025

Leo ni Jumatano 15 Mfunguo Saba Rabiuthani 1447 Hijria sawa na 8 Oktoba 2025 Miladia.

Katika siku kama ya leo miaka 114 iliyopita, vita vya Balkan vilianza kwa ushiriki wa Bulgaria, Serbia na Ugiriki dhidi ya Utawala wa Othmania. Ufalme wa Othmania kwa miaka kadhaa mtawalia ulikuwa umefanikiwa kuyafanya maeneo mengi ya magharibi mwa Asia, kaskazini mwa Afrika na mashariki mwa Ulaya kuwa chini ya udhibiti wake na hivyo ukawa umetanua utawala wake. Vuguvugu la kulitaka kujitenga nchi zilizokuwa chini ya utawala huo lilikuwa likipelekea kutokea vurugu mara kwa mara na vita vya Balkan ni moja ya harakati hizo.

 

Miaka 97 iliyopita katika siku kama ya leo mwafaka na tarehe 16 Mehr mwaka 1307 Hijiria Shamsia kufuatia upinzani wa Sayyid Hassan Mudarres dhidi ya udikteta wa Reza Khan Pahlawi, mtawala huyo aliwaamuru askari wake wavamie nyumba ya Ayatullah Muddares, kumpiga na kumjeruhi na kisha akahamishiwa nje ya mji wa Tehran. Askari hao pia waliwatia nguvuni watu wa familia ya mwanazuoni huyo. Mwishowe Ayatullah Mudarres alibaidishwa katika mji wa Kashmar kaskazini mashariki mwa Iran na kuuawa shahidi na askari wa Reza Khan mwaka 1316 Hijiria Shamsia. ***

Sayyid Hassan Mudarres

 

Katika siku kama ya leo miaka 54 iliyopita, Sultan al-Waidhin Shirazi, mhakiki, mwandishi wa vitabuu na mtoa waadhi mashuhuri  wa Kiislamu Aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 75, Sayyid Muhammad Shirazi ambaye nim toto wa Ashraf al-Waidhin Hj Ali Akbar alizaliwa mjini Tehran na kusoma masomo ya msingi katika mji huo. Akiw ana umri wa miaka 12 alifuataana na baba yake Kwenda Iraq na akiwa katika mji wa Karbala ajishughulisha na kusoma kwa muda wa miaka 2. Baadaye akiwa na lengo la kujiendeleza zaidi kielimu alifanya safari katika mataifa ya Syria, Palestina, Jordan, Misri na India. Akiwa katika mataifa hayo alifanya midahalo ya kidini na kimadhehhebu na makundi mbalimbali ya Kiyahudi, Kikristo, Masuni na kadhalika.

Sultan al-Waidhin Shirazi

 

Katika siku kama ya leo miaka 38 iliyopita, utawala wa Baath wa Iraq uliushambulia kwa mabomu ya kemikali mji wa Sumar wa Iran. Raia wengi waliuawa shahidi katika shambulio hilo. Katika kkipindi cha miaka 8 ya vita vya kichokozi ilivyoansisha dhidi ya Iran, utawala wa Saddam ulitumia mara kkadhhaa silaha za kemikali. Takribani raia laki moja waliuawa shahidi au kujeruhiwa katika tukio hilo la kinyama. ***

 

Miaka 20 iliyopita katika siku kama ya leo, mtetemeko mkubwa wa ardhi uliokuwa na ukubwa wa 7.8 kwa kipimo cha Rishta uliyakumba maeneo ya kaskazini mashariki mwa Pakistan. Kitovu cha mtetemeko huo kilikuwa katika mji wa Muzaffarabad. Watu wapatao 90 elfu walipoteza maisha yao na wengine milioni 3 na laki 6 kubaki bila makazi kufuatia mtetemeko huo.