Jumanne, 16 Disemba, 2025
Leo ni Jumanne tarehe 25 Mfunguo Tisa Jamadithani 1447 Hijria mwafaka na tarehe 16 Disemba 2025.
Katika siku kama ya leo miaka 250 iliyopita, Jane Austen, mwandishi mwanamke wa Uingereza alizaliwa.
Hakuishi kwa zaidi ya miaka 42 kwani aliaga dunia 1817. Hata hivyo, Jane Austen alikuwa na taathira kubwa mno katika fasihi ya Kiingereza na hata Ulaya kwa ujumla. ***
Siku kama hii ya leo miaka 162 alizaliwa George Santayana, mwanafalsafa na mwandishi wa Kihispania.
Akiwa na umri wa miaka 9 George Santayana alihajiri pamoja na familia yake na kuelekea Marekani. Baada ya kukamilisha masomo ya nmsingii na ya sekondari alijiunga na Chuo Kikuu cha Havard. Pamoja na hayo katika kipindi chake cha kuishi Marekani kwa muda wa miaka 41 alikuwa amejitenga na hakuwa na furaha.
Hatimaye mwaka 1913 Santayana aliekea barani Ulaya na kujifunza falsafa katika mataifa ya Uingereza na Ujerumani na kisha baadaye nchinii Italia.
Siku kama ya leo miaka 138 iliyopita Ayatullah Mirza Muhammad Hassan Shirazi alitoa fatuwa maarufu ya kuharamisha tumbaku na sigara ili kuzuia uporaji uliokuwa ukifanywa na wakoloni wa Kiingereza katika nchi za Kiislamu.
Fatua hiyo ilitolewa baada ya mfalme Nasiruddin Shah wa Iran kutia saini mkataba wa kuipa kampuni moja ya utawala wa kikoloni wa Uingereza mamlaka ya kuuza na kununua tumbaku ya Iran kwa kipindi cha miaka 50.
Jina la Mirza Shirazi ni mashuhuri mno kutokana na fatua hiyo ya kuharamisha tumbaku. Fatua yake hiyo ya kuharamisha tumbaku na matumizi ya sigara, bidhaa ambayo ilikuwa imehodhiwa na Uingereza, ilitoa pigo kubwa kwa ukoloni wa Uingereza nchini Iran. Vilevile fatua hiyo ilitambuliwa kuwa mapambano ya moja kwa moja dhidi ya utawala wa Shah na ukoloni wa Uingreza nchini Iran na iliandaa uwanja wa mapambano ya baadaye ya wananchi wa Iran dhidi ya dhulma, ukandamizaji na ukoloni wa wageni.
Siku kama ya leo miaka 75 iliyopita ilianza harakati ya kupigania uhuru ya watu wa Cyprus kwa shabaha ya kuhitimisha ukoloni wa Waingereza kisiwani humo.
Kisiwa cha Cyprus kilichoko katika Bahari ya Miditerranean kiliwekwa chini ya utawala wa Kiothmania katika karne ya 16.
Mwaka 1925 Uingereza ilikiunganisha kisiwa hicho na makoloni yake na tangu wakati huo kulitokea mapigano baina wakazi wa kisiwa hicho yaani Waturuki na Wagiriki. Hatimaye Cyprus ilipata uhuru mwaka 1974 baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa na Wagiriki huku Waturuki wa kisiwa hicho wakidhibiti eneo la kaskazini la nchi hiyo.

Katika siku kama hii ya leo miaka 34 iliyopita Kazakhstan ilijitangazia uhuru baada ya kudhihiri dalili za kusambaratika Urusi ya zamani.
Wakazaki ambao wanaunda jamii kubwa zaidi nchini humo na ambao ni kutoka makabila ya Waturki na Wamongoli, katika karne ya 17 miladia, waligawanyika katika sehemu tatu za tawala kubwa za kisultani.
Mwanzoni mwa karne ya 18 taratibu waliwekwa chini ya udhibiti wa Warusi na wakati huo hususan katika karne ya 19, wakazaki hao wakiwa pamoja na watu wa maeneo mengine ya Asia ya kati, walijiunga na dini ya Kiislamu.

Siku kama hii ya leo miaka 27 iliyopita Mahakama ya Rufaa ya Paris ilimhukumu kifungo na kumtoza faini mwanafalsafa na msomi mashuhuri wa nchi hiyo, Roger Garaudy, kwa kosa eti la kukana jinai dhidi ya binadamu katika kitabu chake cha 'The Founding Myths of Israeli Politics'.
Katika kitabu hicho msomi huyo Mfaransa alithibitisha kisayansi na kwa hoja madhubuti kwamba Wazayuni walishirikiana na Manazi katika Vita vya Pili vya Dunia. Vilevile amethibitisha kwa hoja na ushahidi kwamba, kwa shabaha ya kutaka kupata uungaji mkono wa kuunda dola bandia la Israel katika ardhi ya Palestina, Wazayuni walikuza na kutia chumvi kupita kiasi jinai zilizofanywa na Adolph Hitler dhidi ya Mayahudi.
Katika kitabu cha 'The Founding Myths of Israeli Politics' Profesa Garaudy anasema, idadi ya Mayahudi milioni 6 inayotajwa na Wazayuni kuwa iliuawa na Wajerumani wa zama za Hitler imetiwa chumvi kupita kiasi kwani jamii ya Wayahudi katika kipindi hicho haikuwa kubwa kiasi hicho.
Msomi huyo alikamatwa na kuhukumiwa kifungo nchini Ufaransa kutokana na maoni yake, suala ambalo limethibitisha urongo wa madai ya demokrasia na uhuru wa maoni nchini Ufaransa.
Miaka 32 iliyopita katika siku kama ya leo alifariki dunia Ayatullah Muhammad Ali Araki, mmoja wa marjaa wakubwa wa taqlidi wa Waislamu, akiwa na umri wa miaka 103.
Mwanzuoni huyo wa Kiislamu alizaliwa katika mji wa Arak katikati mwa Iran na kujifunza elimu ya dini kwa maulamaa wakubwa hususan Ayatullahil Udhma Hairi.
Ayatullah Muhammad Ali Araki alifundisha katika chuo kikuu cha kidini cha Qum kwa kipindi cha miaka 35 na kulea wanazuoni na wasomi hodari. Mwanazoni huyo mkubwa wa Kiislamu amezikwa katika Haram tukufu ya Maasuma (as) katika mji mtakatifu wa Qum. ***
Miaka 28 katika siku kama ya leo, iliyopita kanali ya televisheni ya Sahar ya Kitengo cha Matangazo ya Ng'ambo cha Shirika la Redio na Televisheni la Iran ilianza kazi zake kwa kurusha matangazo ya lugha za Kiarabu, Kiazari, Kibosnia, Kituruki, Kifaransa, Kiingereza na Kiurdu.
Televisheni za kanali hiyo zinatayarisha na kurusha matangazo mbalimbali yanayolenga familia katika masuala ya kijamii, kisiasa, filamu, sinema za matukio ya kweli, masuala ya kiuchumi na kadhalika.
Vilevile televisheni hizo huakisi habari za matukio mbalimbali ya kieneo na kimataifa.