Dec 05, 2017 02:41 UTC
  • Jumanne tarehe 5 Disemba, 2017

Leo ni Jumanne tarehe 16 Mfunguo Sita Rabiul Awwal 1439 Hijria sawa na tarehe 5 Disemba 2017 Miladia.

Siku kama ya leo miaka 1438 kwa mujibu wa baadhi ya mapokezi ya historia, Swala ya kwanza ya Ijumaa iliswaliwa na Mtume Muhammad (saw) baada ya mtukufu huyo kuhama mji wa Makka. Baada ya kuwasili katika eneo la Bani Salim bin Auf kwa jina la Quba karibu na Madina wakati wa adhuhuri, Mtume (saw) alitoa hotuba na kusimamisha Swala ya Ijumaa mahala hapo. Wanahistoria wanasema hiyo ilikuwa Swala ya kwanza ya Ijumaa katika Uislamu. Hatua hiyo pia inaonesha umuhimu wa ibada hiyo ya kiroho na kisiasa ambayo Bwana Mtume aliamua kuitekeleza mara tu baada ya kuwasili karibu na mji wa Madina.

Miaka 182 iliyopita katika siku kama ya leo, Mirza Abul-Qassim Qaim Maqam Farahani mmoja wa waandishi na wanasiasa wa Iran aliauawa katika kipindi cha utawala wa Qajar. Aliteuliwa kuwa kaimu wa mrithi wa kiti cha ufalme wa Qajar na baadaye kuchaguliwa kuwa Kansela wa Muhammad Shah. Qaim Maqam Farahani alifanya huduma na kuchukua hatua nyingi za marekebisho nchini Iran. Hata hivyo wasiomtakia mema wa ndani ya Iran na wakoloni wa nje ambao hawakufarahishwa na mambo aliyokuwa akiyafanya yaliyokuwa yakipingana na maslahi yao haramu waliandaa uwanja wa kumuua mwanasiasa huyo.

Mirza Abul-Qassim Qaim Maqam Farahani

Katika siku kama ya leo miak 147 iliyopita, aliaga dunia Alexander Dumas mwandishi mtajika wa Kifaransa. Mwandishi huyo ambaye ni mashuhuri pia kwa jina la Dumas Baba baada ya kumaliza masomo yake aliajiriwa katika ofisi moja ya kiwanda kama katibu kutokana na kuwa na hati nzuri.

Alexander Dumas

Siku kama ya leo miaka 143 iliyopita, Iran ilijiunga na Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu. Jitihada za awali za Iran kutaka kujiunga na shirika hilo zinarejea nyuma katika kipindi cha utawala wa Mfalme Nassereddin Shah Qajar. Katika kipindi cha utawala wake, Disemba 1874 Iran iliukubali mkataba uliopasishwa Geneva Uswisi, lakini licha ya kupita miaka kumi tangu isaini mkataba huo, utawala wake haukuchukua hatua yoyote ile ya kuasisi taasisi au jumuiya ambayo ikitekeleza hati ya mkataba huo hapa Iran.

hirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu

 

Tags