-
Mkutano wa pili wa Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa mataifa jirani na Afghanistan+Russia waanza Tehran
Oct 27, 2021 04:42Mkutano wa pili wa Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa mataifa jirani na Afghanistan+Russia umeanza kufanyika hapa mjini Tehran kwa shabaha ya kujadili changamoto mbambali zinazoikabili nchi hiyo baada ya majeshi ya Marekani kuondoka nchini humo na wanamgambo wa Taliban kuchukua hatamu za uongozi wa nchi.
-
Iran: Tunaendelea kufanya mashauriano ya kiusalama na serikali mpya ya Afghanistan
Oct 26, 2021 08:57Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran inaendelea kufanya mashauriano na serikali mpya ya Afghanistan hasa katika masuala ya kuleta amani, utulivu na usalama wa kudunu nchini humo.
-
Sisitizo la Pakistan la kutokuweko makubaliano baina yake na Marekani ya operesheni za kijeshi nchini Afghanistan
Oct 24, 2021 23:01Serikali ya Pakistan imekanusha ripoti za vyombo vya habari zinazoeleza kufikiwa makubaliano kati yake na Marekani kwa ajili ya kufanya operesheni za kijeshi na kijasusi nchini Afghanistan.
-
DAESH lakiri kuhusika na hujuma ya kuripua kinu cha umeme mjini Kabul, Afghanistan
Oct 23, 2021 04:18Kundi la kigaidi na ukufurishaji la DAESH (ISIS) limekiri kuwa ndilo lililohusika na shambulio la kinu kikuu kinachozalisha umeme katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.
-
Kikao cha Moscow kuhusu Afghanistan na juhudi za kurejesha uthabiti nchini humo
Oct 22, 2021 09:36Kikao cha Moscow kuhusu Afghanistan kilifanyika siku ya Jumatano ya tarehe 20 Oktoba kwa uwenyekiti wa Russia katika mji mkuu huo wa nchi hiyo.
-
Sisitizo la Iran la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kuwa na mchango amilifu zaidi nchini Afghanistan
Oct 19, 2021 22:51Hussein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, lengo la genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh huko Afghanistan ni kuchochea chuki na uadui wa kimadhehebu na ameitaka Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC ilaani vikali vitendo vya kinyama vya Daesh.
-
Mjumbe maalumu wa Marekani katika masuala ya Afghanistan ajiuzulu
Oct 19, 2021 04:11Zalmay Khalilzad, anayetazamwa kama nembo na kielelezo kikubwa zaidi cha kufeli kidiplomasia Marekani nchini Afghanistan amejiuzulu wadhifa wake wa mjumbe maalumu wa Washington katika masuala ya nchi hiyo.
-
Wanafunzi, wanavyuoni wa kidini Iran walaani mauaji ya Waislamu Afghanistan
Oct 18, 2021 00:22Wahadhiri na wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Kidini katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran wamefanya maandamano makubwa ya kulaani ongezeko la mashambulio ya kigaidi yanayolenga misikiti ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Afghanistan.
-
Jumuiya ya Kutetea Wahanga wa Ugaidi: Ugaidi unatumiwa kulinda maslahi ya madola ya kibeberu
Oct 16, 2021 22:56Jumuiya ya Kutetea Wahanga wa Ugaidi yenye makao yake nchini Iran imetangaza kuwa, ugaidi umekuwa ukitumiwa kama fimbo na wenzo wa kulinda na kupanua maslahi ya madola ya kibeberu na wala hauna mfungamano na dini wala madhehebu yoyote ya dini.
-
Mlipuko katika msikiti wa Washia katika mji wa Qandahar, Afghanistan
Oct 16, 2021 08:34Makumi ya watu waliokuwa katika Swala ya Ijumaa wameuawa shahidi na wengine karibu ya mia moja wamejeruhiwa katika milipuko miwili iliyotokea jana Ijumaa katika Msikiti wa Bibi Fatima katika mji wa Qandahar Afghanistan. Hii ni mara ya pili kwa Msikiti wa Washia kukumbwa na milipuko huko Afghanistan katika muda wa wiki moja.