-
Jeshi la Sudan lakanusha kushambulia msafara wa misaada wa WFP katika jimbo la Darfur
Aug 22, 2025 10:03Jeshi la Sudan (SAF) limekanusha madai yaliyotolewa wapiganaji wa Vikosi vya Usaidzi wa Haraka (RSF) kuwa limefanya mashambulizi ya angani dhidi ya msafara wa misaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) uliokuwa unapeleka misaada Darfur.
-
Maandamano ya kutaka kulindwa wanahabari wa Gaza yafanyika Afrika Kusini
Aug 18, 2025 06:48Waandishi wa habari wa Afrika Kusini na wafanyakazi wa vyombo vya habari wameongoza maandamano huko Sea Point jijini Cape Town, wakishinikiza kupewa ulinzi zaidi waandishi wa habari wa Palestina huko Gaza, sanjari na kutangaza mshikamano na wenzao waliouawa katika ukanda huo wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
-
Katika muda wa juma moja, watu 63 wameaga dunia kwa lisheduni mjini El-Fasher, Sudan
Aug 11, 2025 10:49Watu wasiopungua 63, wengi wao wakiwa wanawake na watoto wamefariki dunia kutokana na upungufu wa lishe katika mji uliozingirwa wa El-Fasher, makao makuu ya jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan.
-
Afrika Kusini yasisitiza tena msimamo wake kuhusu mauaji ya kimbari ya Israel, Gaza
Aug 10, 2025 09:22Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini kwa mara nyingine tena amesisitiza kuhusu msimamo wa nchi hiyo katika faili la kesi ya mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni huko Gaza na kusema: Afrika Kusini inaitaka Israel isimamishe vita haraka iwezekanavyo huko Gaza, iruhusu misaada ya kibinadamu kuingia katika eneo hilo, iache kulikalia kwa mabavu eneo hilo na iache kuiaadhibu jamii ya Wapalestina.
-
Je, Afrika Kusini inafanya nini kukabiliana na ushuru mpya wa kibiashara wa Marekani?
Aug 07, 2025 08:19Wizara ya Biashara ya Afrika Kusini imetangaza kuwa imechukua hatua kadaa mpya za kukabiliana na ushuru mpya wa kibiashara wa Marekani.
-
Rais wa Afrika Kusini ajibu bwabwaja na vitisho vya Trump
Jul 08, 2025 13:39Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amejibu matamshi ya vitisho na ubabe ya Rais wa Marekani, Donald Trump ambaye hivi karibuni alitishia kuongeza ushuru wa asilimia kwa nchi ambazo zinajiegemeza na kufungamana na "sera za kupambana na Marekani" za jumuiya ya kiuchumi ya BRICS.
-
Rais wa Afrika Kusini: Mazungumzo ya kitaifa yataendelea bila mshirika wa muungano
Jul 04, 2025 15:19Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema kuwa mazungumzo ya kitaifa yenye lengo la kuimarisha umoja na kuiunganisha nchi baada ya uchaguzi wa mwaka jana yataendelea bila mshirika mkuu katika serikali ya mseto ya nchi hiyo.
-
Chama cha DA cha Afrika Kusini chajiondoa kwenye mazungumzo ya kitaifa
Jun 29, 2025 02:44Chama cha Democratic Alliance cha nchini Afrika Kusini kimejiondoa kwenye mazungumzo ya kitaifa hata hivyo hakijajitoa katika serikali ya mseto baada ya Rais wanchi hiyo Cyril Ramaphosa kumfuta kazi Naibu Waziri wake mmoja. Haya yameelezwa na kiongozi wa chama hicho John Steenhuisen.
-
Afrika Kusini yazika miili 30 iliyotelekezwa kwenye mgodi wa dhahabu
Jun 11, 2025 07:19Afrika Kusini jana Jumanne ilifanya maziko ya kwanza ya 'kimaskini' ya miili 30 ambayo haikuchukuliwa na jamaa zao, baada ya kupatikana kwenye mgodi wa dhahabu uliotelekezwa huko Stilfontein, mkoa wa Kaskazini Magharibi mwezi Januari mwaka huu.
-
Afrika Kusini yaanza kuchunguza jinai za enzi za 'apartheid'
May 31, 2025 10:45Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amemteua Jaji mstaafu wa Mahakama ya Kikatiba, Sisi Khampepe kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Ukweli na Maridhiano (TRC) ya kuchunguza ucheleweshaji wa mashtaka na uchunguzi wa jinai zilizofanyika enzi za ubaguzi wa rangi (apartheid) nchini humo.