-
Yemen yakadhibisha madai ya Saudia na Imarati ya kuhusika Ansarullah katika shambulio kubwa huko Ma'rib
Jan 21, 2020 08:41Harakati ya wapiganaji wa Ansarullah wa Yemen imekanusha madai ya Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) kwamba ndiyo iliyohusika na shambulio kali la kombora katika ngome za wanamgambo wenye mfungamano na Riyadh katika mji wa Ma'rib kusini mwa Yemen.
-
Answarullah ya Yemen: Damu ya Jenerali Qasem Soleimani imeainisha njia ya kuhitimisha uwepo wa Marekani katika eneo
Jan 06, 2020 10:07Salim Al-Mughlis, Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa wa Harakati ya Wananchi ya Answarullah ya nchini Yemen amesema kuwa shahidi Qassem Soleimani ameainisha njia ya kuhitimisha uwepo wa Marekani katika eneo hili.
-
Muhammad al Houthi: Saudi Arabia inapasa kukubali amani ili kuhitimisha matatizo ya kiuchumi yanayoikabili
Dec 29, 2019 04:31Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen amesema kuwa Saudi Arabia inapasa kukubali amani ili kupunguza gharama kubwa za kuendesha vita huko Yemen ambazo zimeipelekea nchi hiyo ikabiliwe na matatizo chungu nzima ya kiuchumi.
-
Dakta Zarif akutana na Naibu Sultani wa Oman na msemaji wa Ansarullah Muscat
Dec 24, 2019 23:25Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amekutana na kufanya mazungumzo na Mohammad Abdul Salam, msemaji wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen nchini Oman.
-
Harakati ya Answarullah ya Yemen: Marekani ndio inazuia kusimamishwa vita
Dec 14, 2019 21:43Mohammed Ali al-Houthi, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi nchini Yemen ameitaja Marekani kuwa ndio kizuizi kikuu cha kutosimamishwa uvamizi na mzingiro dhidi ya taifa hilo la Kiarabu.
-
Harakati ya Ansarullah yakaribisha kuondoka wanajeshi wa Sudan huko Yemen
Dec 08, 2019 23:08Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen ameunga mkono uamuzi wa Waziri Mkuu wa Sudan wa kuondoa wanajeshi wa nchi hiyo walioko Yemen.
-
Yemen yaikosoa China kwa kuwa na msimamo wa undumilakuwili kuhusiana na nchi hiyo
Dec 01, 2019 09:31Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen ameikosoa China kwa kuwa na msimamo unaogongana na wa undumilakuwili kuhusiana na nchi hiyo, baada ya ndege moja isiyo na rubani iliyotengezwa China kutunguliwa kaskazini magharibi mwa Yemen.
-
Yemen: Saudia inafanya juhudi za kuanzisha mawasiliano na Answarullah
Nov 07, 2019 09:20Mshauri wa Baraza Kuu la Kisiasa nchini Yemen anayehusika na masuala ya kidiplomasia ameelezea juhudi zinazofanywa na Saudia kwa ajili ya kuanzisha uhusiano na harakati ya wananchi ya Answarullah ya nchi hiyo.
-
Ansarullah: Chaguo la kijeshi haliwezi kuleta amani Yemen na katika eneo
Oct 29, 2019 03:51Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameonya kuhusu uvamizi na mashambulizi yanayofanywa na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya nchi hiyo na kusisitiza kuwa, chaguo la kijeshi katu haliwezi kurejesha amani nchini Yemen na katika eneo.
-
Ansarullah yaonya askari wa Marekani walioko Saudia; jifunzeni kwa Vietnam
Oct 13, 2019 04:32Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen, Muhammad Ali al-Houthi ameitaka Marekani ijifunze kutokana na vita vilivyojiri huko Vietnam kuanzia mwaka 1954-1975 na kuisababisha Marekani maafa na hasara kubwa.