Harakati ya Ansarullah yakaribisha kuondoka wanajeshi wa Sudan huko Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i57757-harakati_ya_ansarullah_yakaribisha_kuondoka_wanajeshi_wa_sudan_huko_yemen
Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen ameunga mkono uamuzi wa Waziri Mkuu wa Sudan wa kuondoa wanajeshi wa nchi hiyo walioko Yemen.
(last modified 2025-11-07T02:31:33+00:00 )
Dec 09, 2019 02:38 UTC
  • Harakati ya Ansarullah yakaribisha kuondoka wanajeshi wa Sudan huko Yemen

Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen ameunga mkono uamuzi wa Waziri Mkuu wa Sudan wa kuondoa wanajeshi wa nchi hiyo walioko Yemen.

Muhammad Ali al Houthi amesema kuwa kurejeshwa nyumbani wanajeshi wa Sudan walioko Yemen kutazuia kuendelea umwagaji damu huko Yemen. Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen amebainisha hayo akijibu matamshi ya Abdallah Hamdok Waziri Mkuu wa Sudan kuhusu suala la kuwaondoa wanajeshi wa nchi hiyo walioko Yemen. 

Abdallah Hamdok, Waziri Mkuu wa Sudan

Waziri Mkuu wa Sudan Ijumaa iliyopita alitangaza kuwa wanajeshi wa Sudan wanapasa kurejea nyumbani na kusisitiza kuwa mgogoro wa Yemen utapatiwa ufumbuzi kwa njia ya kisiasa na mazungumzo na si kwa hatua za kijeshi. Alisema kuwa, Sudan itawasadia ndugu zao wa Yemen kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo. 

Yahya Saree Msemaji wa Jeshi la Yemen mwezi uliopita alitangaza kuwa wanajeshi wa Sudan elfu nane wameuawa na kujeruhiwa katika vita huko Yemen wakishirikiana bega kwa bega na muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia.