-
Ansarullah: Hatutasitisha uungaji mkono wetu kwa watu wa Gaza
Apr 27, 2025 07:34Naibu mkuu wa taasisi ya habari la Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza katika taarifa yake kwamba, kwa hali yoyote ile msaada na uungaji mkono wa harakati hiyo kwa wananchi wanaodhulumiwa wa Ukanda wa Gaza hautasita.
-
Ansarullah: US inashajiisha mauaji ya kimbari Gaza, yataka Wapalestina wapewe silaha
Apr 18, 2025 06:30Kiongozi wa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen amesema Marekani inaihimiza na kuishajiisha Israel kuendeleza vita vya mauaji ya halaiki huko Gaza na kusisitiza kuwa Washington ni mshiriki wa utawala wa Kizayuni katika mauaji hayo ya kimbari.
-
Yemen yalishambulia kwa droni eneo la kijeshi la Israel, Tel Aviv, yatungua droni ya US Sa'daa
Apr 05, 2025 07:19Vikosi vya Ulinzi vya Yemen (YAF) vimefanya operesheni ya kijeshi kulenga eneo la jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji wa Yafa kwa kutumia ndege isiyo na rubani ya Yaffa iliyotengenezwa ndani ya Yemen, na kuiangusha pia ndege isiyo na rubani ya Marekani aina ya Giant Shark F360 katika Mkoa wa Sa'daa.
-
Israel imeua zaidi ya Wapalestina 150 tangu usitishaji vita ulipoanza kutekelezwa Ghaza Januari 19
Mar 16, 2025 10:52Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Serikali ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza imetangaza kuwa, zaidi ya Wapalestina 150 wameuliwa shahidi na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel- tangu makubaliano ya kusitisha mapigano yalipoanza kutekelezwa katika eneo hilo Januari 19 mwaka huu-, wakiwemo 40 waliouawa katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.
-
Ansarullah: Matakfiri Syria ni vikaragosi vya madola ajinabi
Mar 10, 2025 11:25Kiongozi wa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen amelaani vikali machafuko mabaya yaliyotokea hivi karibuni katika eneo la pwani ya magharibi mwa Syria na kusisitiza kuwa, mbali na kuwa ghasia hizo ni tishio kwa wahusika wa jinai hizo na walezi wao, lakini pia ni somo kwa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu.
-
Yemen: US kuiweka Ansarullah katika orodha ya ugaidi haina uhalali wowote
Mar 07, 2025 02:33Afisa mmoja mwandamizi wa Yemen amepuuzilia mbali hatua ya Marekani ya kuitambua Harakati ya Muqawama ya Ansarullah kama kundi la kigaidi, akisema uamuzi huo hauna uhalali wowote.
-
Ansarullah: Israel inatumia uungaji mkono wa US kukiuka makubaliano
Mar 01, 2025 07:13Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema Yemen inafuatilia kwa karibu utekelezwaji wa makubaliano ya usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza na kuongeza kuwa, inashuhudia namna "adui Mzayuni" anakwepa kutekeleza majukumu yake.
-
Balozi wa UN aionya US kuiweka Ansarullah kwenye orodha ya magaidi
Feb 14, 2025 12:08Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen, Hans Grundberg ameonya kuhusu athari mbaya za Marekani kuitambua Harakati ya Ansarullah ya Yemen kuwa kundi la kigeni la kigaidi, kutokana na mashambulizi ya kundi hilo la Muqawama ya kulipiza kisasi dhidi ya maeneo ya Israel.
-
Ansarullah ya Yemen: Marekani haina haki ya kuzihukumu nchi zingine
Jan 24, 2025 09:19Harakati ya Ansarullah ya Yemen iimetoa radiamali kwa hatua ya Marekani ya kuiweka Yemen katika orodha ya magaidi na kubainisha kwamba, Washington ambayo inahusika na mauaji ya Wapalestina na wasio na hatia haina haki ya kuzihukumu nchi zingine.
-
Trump akosolewa kwa kuirejesha Ansarullah katika 'orodha ya magaidi'
Jan 23, 2025 07:49Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekosoa vikali hatua ya Rais wa Marekani, Donald Trump ya kuanzisha mchakato wa kuirejesha Harakati ya Ansarullah ya Yemen katika orodha ya Washington ya makundi ya 'kigaidi'.