-
Shakhsia 200 duniani: Utawala wa kibaguzi wa Israel utokomezwe, kuupa kinga ya kutoadhibiwa kukomeshwe
Aug 09, 2025 23:12Zaidi ya shakhsia 200 mashuhuri ulimwenguni kote, wakiwemo viongozi wa kisiasa, wasomi, watetezi wa haki za binadamu, waandishi wa habari, wanazuoni wa kidini na watu mashuhuri wa kiutamaduni, wameandika barua ya pamoja kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakitaka "kutokomezwa ubaguzi wa rangi wa apathaidi" na "kukomeshwa kinga ya kutoadhibiwa" kwa jinai na uhalifu unaofanywa na utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya watu wa Palestina.
-
Shambulio la kombora la Yemen lailazimisha Israel ifunge anga yake
Jul 22, 2025 02:19Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeripoti kuwa, Israel imelazimika kufunga uwanja wa ndege wa Ben Gurion na anga yake katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu kufuatia kuvurumishwa kwa kombora kutoka Yemen.
-
Ansarullah: Kuteswa, kuuawa kwa njaa watu wa Gaza ni ‘fedheha’ kwa ulimwengu wa Kiarabu, Kiislamu
Jul 21, 2025 03:31Kiongozi wa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen amelaani vikali nchi za Kiarabu na Kiislamu duniani kwa kushindwa kwao kutoa jibu mwafaka mkabala wa hatua ya utawala wa Israel ya kuwaua kwa makusudi Wapalestina katika Ukanda wa Gaza kwa kutumia njaa.
-
Ansarullah yaionya Israel: Haiyumkiniki kufungua bandari ya Eilat
Jul 10, 2025 17:19Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ametangaza kuwa, ni jambo lisilowezekana kufunguliwa tena kwa bandari ya Eilat (Umm al-Rashrash), akisisitiza msimamo thabiti wa Yemen wa kuendelea kutekeleza vikwazo vya baharini dhidi ya utawala ghasibu wa Israel katika Bahari Nyekundu, Ghuba ya Aden na Bahari ya Arabia.
-
Ansarullah kupanua wigo wa operesheni zake dhidi ya Israel
Jun 11, 2025 03:48Harakati ya Ansarullah ya Yemen imetangaza kuwa itapanua wigo wa operesheni zake dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Yemen yaiwekea mzingiro Bandari ya Haifa ili kuiunga mkono Palestina
May 20, 2025 22:56Yemen imetangaza habari ya kuifunga Bandari ya Haifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na kupachikwa jina bandia la Israel, ili kuwaunga mkono wananchi wa Palestina na kujibu mashambulizi yanayoendelea kufanywa na Wazayuni dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Ansarullah: Hatutasitisha uungaji mkono wetu kwa watu wa Gaza
Apr 27, 2025 04:04Naibu mkuu wa taasisi ya habari la Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza katika taarifa yake kwamba, kwa hali yoyote ile msaada na uungaji mkono wa harakati hiyo kwa wananchi wanaodhulumiwa wa Ukanda wa Gaza hautasita.
-
Ansarullah: US inashajiisha mauaji ya kimbari Gaza, yataka Wapalestina wapewe silaha
Apr 18, 2025 03:00Kiongozi wa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen amesema Marekani inaihimiza na kuishajiisha Israel kuendeleza vita vya mauaji ya halaiki huko Gaza na kusisitiza kuwa Washington ni mshiriki wa utawala wa Kizayuni katika mauaji hayo ya kimbari.
-
Yemen yalishambulia kwa droni eneo la kijeshi la Israel, Tel Aviv, yatungua droni ya US Sa'daa
Apr 05, 2025 03:49Vikosi vya Ulinzi vya Yemen (YAF) vimefanya operesheni ya kijeshi kulenga eneo la jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji wa Yafa kwa kutumia ndege isiyo na rubani ya Yaffa iliyotengenezwa ndani ya Yemen, na kuiangusha pia ndege isiyo na rubani ya Marekani aina ya Giant Shark F360 katika Mkoa wa Sa'daa.
-
Israel imeua zaidi ya Wapalestina 150 tangu usitishaji vita ulipoanza kutekelezwa Ghaza Januari 19
Mar 16, 2025 07:22Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Serikali ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza imetangaza kuwa, zaidi ya Wapalestina 150 wameuliwa shahidi na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel- tangu makubaliano ya kusitisha mapigano yalipoanza kutekelezwa katika eneo hilo Januari 19 mwaka huu-, wakiwemo 40 waliouawa katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.