-
Bandari ya Israel kuwatimua nusu ya wafanyakazi kutokana na hujuma za Yemen
Mar 22, 2024 10:55Asilimia 50 ya wafanyakazi katika bandari ya Eilat ya utawala wa Kizayuni wa Israel wapo hatari ya kupigwa kalamu nyekundu kutokana na athari za mashambulizi ya vikosi vya Yemen katika Bandari Nyekundu.
-
Yemen yashambulia meli za Marekani na Israel katika Bahari ya Hindi
Mar 16, 2024 07:38Vikosi vya Jeshi la Yemen vimetangaza habari ya kupanua operesheni zao kwa kuzishambulia meli za Marekani na utawala haramu wa Israel katika maji ya Bahari ya Hindi.
-
Ansarullah: Operesheni za kushambulia meli zenye uhusiano na Israel zitapanuliwa hadi Bahari ya Hindi
Mar 15, 2024 07:41Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen, Sayyid Abdul Malik Al-Houthi amesema askari wa jeshi la nchi hiyo wataendelea na operesheni zao za kujibu mapigo dhidi ya meli za kibiashara zenye uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel, kwa kuzizuia meli hizo kupita hata kwenye eneo la maji ya Bahari ya Hindi na Rasi ya Tumaini Jema.
-
Ansarullah ya Yemen: Baada ya tuliyoizamisha, tutaendelea kuzishambulia meli za Uingereza katika Bahari Nyekundu
Mar 04, 2024 09:07Yemen imeapa kuwa itaendelea kuzishambulia meli za Uingereza katika Bahari Nyekundu ili kuwaunga mkono Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza, ambao wamekuwa wakiandamwa na vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendeshwa na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa muda wa miezi mitano sasa.
-
Ansarullah: US kuiasa China iingilie kadhia ya Bahari Nyekundu ni ishara ya kufeli
Feb 02, 2024 07:49Kiongozi wa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen amesema juhudi za Washington za kutafuta usaidizi na upatanishi wa China ili iwaombe Wayemen wasimamishe mashambulizi dhidi ya meli za Marekani na Uingereza zinazopita Bahari Nyekundu zinaonesha namna madola hayo mawili ya kibeberu yalivyofeli katika mipango yao.
-
Safari za majini katika Ghuba ya Tumaini Jema zaongezeka kufuatia mashambulizi ya jeshi la Yemen katika Bahari Nyekundu
Jan 28, 2024 03:07Kufuatia mashambulizi yanayoendelea kufanywa na vikosi vya ulizi vya Yemen katika Bahari Nyekundu dhidi ya dhidi ya meli za utawala wa Kizayuni na za nchi waitifaki zinazoelekea upande wa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina (Israel), meli nyingi sasa zimemua kukwepa Mfereji wa Suez na kuzunguka Ghuba ya Tumaini Jema (Cape of Good Hope) ya Afrika Kusini.
-
Upinzani wa China kwa hatua ya Marekani ya kuishambulia kijeshi Yemen
Jan 27, 2024 02:34Wang Wenbing, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halijatoa kibali kwa mtu yeyote kutumia nguvu dhidi ya Yemen, akimaanisha hujuma na mashambulio ya kijeshi yanayofanywa na Marekani na Uingereza dhidi ya ngome na vituo vya harakati ya Ansarullah ya Yemen.
-
Ansarullah yaitaka UN iwaondoe Yemen wafanyakazi wake raia wa US, UK
Jan 25, 2024 11:12Harakati ya Ansarullah imeziagiza Marekani na Uingereza ziwaondoea nchini Yemen raia wake wanaoufanyia kazi Umoja wa Mataifa katika mji mkuu wa nchi hiyo ya Kiarabu, Sana'a.
-
Iran yaikosoa US kwa kuiweka Ansarullah katika orodha ya 'ugaidi'
Jan 19, 2024 03:30Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali hatua ya Marekani ya kuiweka Harakati ya Ansarullah ya Yemen kwenye orodha ya kile inachokiita "makundi ya kigaidi" na kueleza kwamba, kitendo hicho ni katika mfululizo wa hatua za Washington za kuuunga mkono utawala wa kigaidi wa Israel.
-
Ansarullah ya Yemen: Ni fakhari kwetu kuitwa magaidi na utawala wa kigaidi wa Marekani kwa sababu ya Palestina
Jan 18, 2024 06:43Ofisi ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen imetoa mjibizo kwa hatua ya Marekani ya kuiweka harakati hiyo kwenye orodha ya kile inachokiita "makundi ya kigaidi" na kueleza kwamba hatua hiyo ya Washington haina thamani wala itibari yoyote.