Jul 19, 2024 13:06 UTC
  • Sayyid Abu Tarabifard
    Sayyid Abu Tarabifard

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema: Shambulio la Yemen dhidi ya Tel Aviv ni onyo linaloitaka Israel ihitimishe mashambulizi ya kinyama ya Wazayuni dhidi ya watu wa Gaza.

Asubuhi ya leo Ijumaa, msemaji wa jeshi la Yemen, Yahya Saree, ametangaza kuwa jeshi hilo limefanya shambulio lililofanikiwa la ndege isiyo na rubani huko Tel Aviv. Katika shambulio hilo, ndege kubwa isiyo na rubani ilitumwa Tel Aviv kutoka baharini katika mwinuko wa chini na baada ya kuvuka tabaka zote za mifumo ya ulinzi ya Israel, imepiga jengo moja karibu na ubalozi wa Marekani mjiini Tel Aviv.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran, Hujjatul Islam Sayyid Mohammad Hasan Abu Tarabifard, amesema: Jeshi la Yemen ambalo limesimama kidete kukabiliana na uchokozi wa ulimwengu wa kibeberu unaoongozwa na Marekani, limeupa fahari na heshima nyingine Umma wa Kiislamu.

Hatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran ameongeza kuwa: Ndege hiyo isiyo na rubani imepiga jengo la karibu na ubalozi wa Marekani mjini Tel Aviv na kutoa onyo la kutaka kukomeshwa mashambulizi ya kinyama ya wavamizi Wazayuni dhidi ya ndugu zetu wa Gaza.

Mtu mmoja ameuawa huku wengine zaidi ya 10 wakijeruhiwa baada ya mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel kushindwa kutungua ndege isiyo na rubani (droni) ya jeshi la Yemen.

Yahya Saree

Brigedia Jenerali Yahya Saree amesema kuwa, shambulio hilo la ndege zisizo na rubani limefanywa kwa ajili ya kuwaunga mkono Wapalestina wanaodhulumiwa huko Gaza na wanamapambano wao mashujaa wa Muqawama, na kulipiza kisasi mauaji yanayofanywa na jeshi la Israel dhidi ya raia wa kawaida katika eneo hilo linalozingirwa.

Tags