Kamanda: Hatutaruhusu hata shibri moja ya ardhi ya Iran itwaliwe
Mkuu wa Jeshi la Iran, Meja Jenerali Amir Hatami, amesisitiza kuwa wanajeshi wa nchi hii hawataruhusu hata shubri moja ya ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu kuporwa.
Leo Ijumaa, Hatami ametembelea kambi ya ndege ya Shahid Lashkari mjini Tehran. Admeli Habibollah Sayyari, Naibu Mkuu wa Jeshi la Iran katika masuala ya Uratibu, na Brigedia Jenerali Hamid Vahedi, Kamanda wa Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIAF), walitathmini utayarifu wa vita wa kambi hiyo kwa pamoja.
"Katika kipindi cha miaka minane ya vita vya Kujihami Kutakatifu, tulidhihirisha kwamba hatutaruhusu hata inchi moja ya ardhi ya Iran kutenganishwa," Hatami amesema, akirejelea Vita vya Iran-Iraq vya miaka ya 1980.
Amesisitiza jukumu la Jeshi la kulinda mamlaka ya ardhi ya nchi, na kusema kwamba vikosi vya jeshi vimejitolea kulinda mfumo wa Kiislamu unaotawala Iran, na pia kuhifadhi mamlaka ya kujitawala na uhuru wa Iran.
Mkuu wa Jeshi la Iran, Meja Jenerali Amir Hatami amesisitiza kuwa, Jeshi la Iran litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa nguvu na azma thabiti.