Yedioth Ahronoth: Israel leo iko mikononi mwa serikali kichaa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i128358
Katika tahariri yake ya leo, Jumanne, gazeti la Yedioth Ahronoth limeshambulia mbinu ya baraza la mawaziri na muungano wa Netanyahu, na kuliita baraza la mawaziri kichaa ambalo lazima lipinduliwe.
(last modified 2025-07-15T10:54:16+00:00 )
Jul 15, 2025 10:54 UTC
  • Yedioth Ahronoth: Israel leo iko mikononi mwa serikali kichaa

Katika tahariri yake ya leo, Jumanne, gazeti la Yedioth Ahronoth limeshambulia mbinu ya baraza la mawaziri na muungano wa Netanyahu, na kuliita baraza la mawaziri kichaa ambalo lazima lipinduliwe.

Yedioth Ahronoth limeandika, mtazamo wa baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu unatupeleka kwenye hali hatari na leo Israel iko mikononi mwa serikali kichaa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Quds (Qodsna), Ron Ben-Yashai, mwandishi wa gazeti la Yedioth Ahronoth, ameandika katika makala yyake ya toleo la leo la gazeti hilo: "Sitaki kulipindua baraza la mawaziri la sasa la Israel kwa ajili ya kujifurahisha, lakini matukio ambayo nimeshuhudia katika siku chache zilizopita yamenifikisha kwenye hitimisho hili, hitimisho ambalo sijawahi kufikia katika maisha yangu yote, ambayo ni kwamba leo Israel iko mikononi mwa serikali ambayo ni kichaa."

Tahariri ya Aharonot inaendelea kueleza: "Baraza la mawaziri lenye hekima kwelikweli, katika kilele cha vita dhidi ya pande saba tofauti, lisingefuatilia kesi ya mapinduzi ya kisheria na, badala ya kufanya maamuzi yenye hatima, lisingetafuta kugawanya jamii kwa njia hii, likipanda mbegu za chuki na mifarakano katika safu za jamii."

Mwandishi wa makala hiyo anaendelea kuuandika: Baraza la mawaziri lenye hekima halingependekeza waakati huuu katika kilele cha vita, kuwaachilia huru vijana 80,000 wanaostahiki utumishi wa kijeshi wa lazima.

Hii ni katika hali ambayo jeshi la Israel linakabiliwa na uhaba wa wanajeshi wasiopungua 10,000 na kusisitiza kuwa linahitaji idadi hiyo ya wanajeshi ili kuhakikisha shughuli zake za usalama.