Umoja wa Mataifa: Hali ya Gaza ni mbaya; kusitisha mapigano haitoshi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i128354-umoja_wa_mataifa_hali_ya_gaza_ni_mbaya_kusitisha_mapigano_haitoshi
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameitaja hali ya Gaza kuwa mbaya na kusema kuwa, usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza pekee hautoshi.
(last modified 2025-07-15T07:22:16+00:00 )
Jul 15, 2025 07:22 UTC
  • Umoja wa Mataifa: Hali ya Gaza ni mbaya; kusitisha mapigano haitoshi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameitaja hali ya Gaza kuwa mbaya na kusema kuwa, usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza pekee hautoshi.

Akielezea hali ya Gaza kuwa ya kutisha, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema eneo hilo linashuhudia vifo na uharibifu usio na kifani katika siku za hivi karibuni, na kwamba hali za kimsingi za utu wa watu wa Gaza zimedhoofishwa.

Afisa huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, wazo la watu milioni 5 wanaoishi bila haki katika ardhi zao ni kinyume cha ubinadamu na sheria za kimataifa.

"Tunahitaji usitishaji vita wa kudumu kabisa huko Gaza," Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema, akisisitiza kuchukuliwa hatua zaidi katika uwanja huo.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada kwa Ajili ya Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limetahadharisha kuhusu hali mbaya ya kiafya huko Gaza Palestina kutokana na ukosefu wa maji ya kunywa na usafi wa mazingira na matokeo ya joto.

Wakati huo huuo, Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imeonya kwamba, mfumo wa chakula wa Gaza uko kwenye ukingo wa kuporomoka kabisa, huku hatua ya kuzuiwa msaada wa kibinadamu kuingia katika eneo hilo kukitishia maisha zaidi.

Huku viwango vya utapiamlo vinavyoongezeka maradufu miongoni mwa watoto na ugavi wa maziwa ya watoto wachanga ukipungua kwa kiwangi cha kutisha, mzozo wa kibinadamu huko Gaza unazidi kuongezeka, na kuweka maelfu ya maisha hatarini.