IAEA: Baada ya miezi michache, Ujerumani itaweza kuunda silaha za nyuklia
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati IAEA Rafael Grossi ametangaza kuwa, Ujerumani inaweza kutengeneza silaha zake za nyuklia ndani ya kipindi cha miezi kadhaa ikiwa itachagua kufanya hivyo. Katika mahojiano na tovuti ya habari ya Poland ya Reczpospolita Grossi amesema Berlin tayari ina nyenzo muhimu za nyuklia, ujuzi na ufikiaji wa teknolojia ya kuunda silaha hizo.
Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu huyo wa IAEA, Ujerumani inaweza kutengeneza bomu la nyuklia ndani ya "muda wa miezi kadhaa," tu ingawa amedai kuwa "hayo ni mawazo ya kidhahania" na kwamba eti nchi za Ulaya zinaendelea kuthibitisha kuwa zinaheshimu Mkataba wa Kuzuia Uenezaji Silaha za Nyuklia (NPT).
Grossi ametoa matamshi hayo na kuzungumzia katika hali ya kawaida uwezo wa Ujerumani wa kuunda silaha za nyuklia endapo itaamua kufanya hivyo huku akitilia mkazo haja ya kufanyika mazungumzo ya kimataifa kuhusu usalama wa nyuklia na umuhimu wa kuzingatia ahadi za kutoeneza silaha za nyuklia, wakati hivi Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zilifanya mashambulio dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran. Mashambulizi hayo yamefanywa kwa kisingizio cha kuizuia Tehran kutengeneza silaha za nyuklia, dali ambalo limekanushwa na IAEA yenyewe na pamoja mashirika ya kijasusi na kiintelijensia ya Marekani.
Mkurugenzi mwenyewe wa wakala wa kimataifa wa nishati ya atomiki hakulaani mashambulio hayo.../