Siku ya ishirini ya mapambano; Wazayuni na Wamarekani watenda jinai katika kinamasi
Vita vya kichokozi vilivyoanzisha na Marekani kwa kushirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, sasa vimeingia siku yake ya ishirini.
Kinyume na makadirio ya awali ya adui, kutofanikiwa kwao kufikia malengo ya kistratejia kumegeuza mambo kutoka mapambano ya kijeshi yaliyotarajiwa kumalizika haraka na kuyafanya yazidi kuwa mgogoro wa kuchosha na wa muda mrefu kwao.
Kwa mujibu wa taarifa ya mwandishi wa Mehr, siku ishirini zimepita tangu kuanza kwa mashambulizi dhidi ya Iran. Wakati Marekani na Israel zilikuwa zinajigamba kuwa ni “vita vya kasi na vifupi”, sasa katika wiki ya tatu ya mapigano wanakabiliwa na hali tofauti kabisa: uimara wa mfumo wa ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu na ugumu mkubwa wa uwanja wa mapambano.
Pamoja na picha za setilaiti kuonyesha uharibifu kwenye vituo vya kijeshi vya Iran, ripoti za uwanjani zinaashiria kuendelea kwa mashambulizi ya Iran dhidi ya malengo muhimu ya maadui katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) na pia dhidi ya vituo vya Marekani katika eneo la Asia Magharibi.
Matukio ya siku ishirini zilizopita yanaonyesha kuwa wataalamu wa kijeshi wa Magharibi walikosea sana katika makadirio yao kuhusu “ustahimilivu wa taifa” na “uwezo wa kuzuia adui” wa Iran.
Wakati mitazamo ya dunia ikifuatilia matukio kwenye medani za mapambano, wachambuzi wa kijeshi wanaona kwamba siku ya ishirini ya vita inaweza kuwa hatua muhimu itakayofungua uwezekano wa kuingia kwa wahusika wapya katika mlinganyo wa vita au kuanzisha mipango ya kusukuma juhudi za amani.
Wakati huo huo, Taarifa ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) imesema kwamba: ndege isiyo na rubani aina ya Orbiter imetunguliwa Jumatano usiku katika anga ya Tehran, na nyingine ya kisasa aina ya Heron katika anga ya Nazarabad, zote mbili ambazo zinamilikiwa na utawala wa Israel, zilikuwa zimebeba silaha na ziliangamizwa kabla ya kutekeleza operesheni zao.
Pia kombora la cruise katika eneo la Kuhin, Qazvin, liliangushwa Jumatano na mfumo mpya wa ulinzi wa anga wa IRGC unaofanya kazi ndani ya mtandao wa pamoja wa ulinzi wa anga wa taifa.
Kwingineko Wimbi la sitini na tatu la operesheni “Ahadi ya Kweli 4” dhidi ya miundombinu ya mafuta inayohusishwa na Marekani katika eneo la Ghuba ya Uajemi limetekelezwa Jumatano kwa ajili ya kuwaenzi mashahidi shujaa wa taasisi za kiusalama.
Katika taarifa namba 43 ya operesheni Ahadi ya Kweli 4, IRGC imetangaza kuwa Jeshi la Wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi limeendelea na “wimbi la sitini na tatu” kwa kulenga vituo ya kijeshi vya Marekani katika nchi za Ghuba ya Uajemi. Opparesheni hiyo imelenga vituo vya “Manhad” na “Al‑Dhafra”, kituo cha helikopta cha “Al‑Udeyri” kinachotumiwa na wanajeshi wa Marekani, pamoja na kituo cha “Mina Salman” ambacho ni makao ya meli za kikosi cha tano cha Marekani.
Katika taarifa namba 44, IRGC imeeleza kuwa: meli kubwa ya kubeba mafuta ya petroli yenye bendera ya “Barbados” ilisimamishwa katika Lango Bahari la Hormuz na kulazimika kubadili mwelekeo baada ya kuamuriwa kufanya hivyo Jeshi la Wanamaji la IRGC. Hivi sasa Iran imechukua udhibiti kamili wa Lango Bahari la Hormuz na hakuna meli inayopita katika eneo hilo bila idhini ya IRGC.