Ujumbe wa Rambirambi wa Kiongozi Muadhamu Kufuatia kuuawa shahidi Dkt.Larijani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137450-ujumbe_wa_rambirambi_wa_kiongozi_muadhamu_kufuatia_kuuawa_shahidi_dkt.larijani
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei, ammetuma ujumbe wa rambirambi kufuatia kuuawa shahidi kwa Dk. Ali Larijani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, pamoja na mwanawe na baadhi ya wenzake.
(last modified 2026-03-19T05:30:17+00:00 )
Mar 19, 2026 05:30 UTC
  • Ujumbe wa Rambirambi wa Kiongozi Muadhamu Kufuatia kuuawa shahidi Dkt.Larijani

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei, ammetuma ujumbe wa rambirambi kufuatia kuuawa shahidi kwa Dk. Ali Larijani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, pamoja na mwanawe na baadhi ya wenzake.

Matini ya ujumbe wa Kiongozi ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

“Wala msidhani wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa wamekufa. Bali wako hai kwa Mola wao, wanapatiwa riziki.” (Qur’ani 3:169)

Kwa masikitiko makubwa nimepokea habari chungu ya kuuawa shahidi kwa Dk. Ali Larijani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa na Mwakilishi wa Kiongozi katika Baraza hilo, pamoja na mwanawe jasiri na baadhi ya wenzake.

Alikuwa mtu mwenye elimu pana, mwenye mtazamo wa mbali, mwenye hekima na mwenye kujitolea, aliyekuwa na tajriba nyingi katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kijeshi, kiusalama, kitamaduni na kiutawala. Karibu nusu karne ya ushiriki wake wa karibu katika ngazi tofauti za mfumo wa Kiislamu ilimfanya kuwa miongoni mwa watu mashuhuri na wenye nafasi ya kipekee.

Mauaji ya mtu wa daraja hili bila shaka yanaonyesha umuhimu wake mkubwa na uadui wa maadui wa Uislamu dhidi yake. Wale wanaopinga Uislamu wanapaswa kujua kwamba kumwaga damu hii katika huduma ya mfumo mkubwa wa Kiislamu kutauimarisha zaidi. Hakika, kila tone la damu linadai kisasi chake, na wauaji wahalifu wa mashahidi hawa watalazimika kulipa gharama ya uhalifu wao hivi karibuni.

Ninatoa rambirambi zangu za dhati kwa mke wake mtukufu, watoto wake wengine, na wanafamilia wote, hususan Ayatullah Ameli Larijani. Ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awape roho za marehemu hawa daraja za juu kabisa.”

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu pia alitoa ujumbe wa rambirambi kufuatia kuuawa shahidi kwa Brigedia Jenerali Gholamreza Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Basij cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).